KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, March 7, 2011

Ujerumani kujadili matumizi ya biofuel






Nchini Ujerumani madereva wamekataa kujaza mafuta yanayotokana na mimea katika magari yao kama sheria mpya ya matumizi ya nishati mbadala inavyotaka nchini humo. Hii inatokana na mkanganyiko wa ni aina gani ya magari yanaweza kutumia mafuta hayo.

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani, Rainer Brüderle, ameitisha mkutano hii leo mjini Berlin kujadili juu ya mzozo huo.Serikali ya Ujerumani haitaki kuachana na mpango wa mamtumizi ya mafuta hayo yanayotokana na mimea na inataka taarifa zaidi zitolewe kwa watumiaji.

Taasisi za magari pamoja na watumiaji nchini Ujerumani wametoa wito kwa viwanda vya magari kutoa maelekezo kwa wateja, kupitia ofisi za makampuni ya magari, iwapo magari yao yanaweza kutumia mafuta hayo ya biofuel. Takriban magari millioni 3 hayawezi kutumia mafuta hayo ya biofuel ambayo yana asilimia kumi ya gesi ya ethanol.





Gaddafi ashambulia waasi upya






Ras Lanuf
Majeshi yanayomtii kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi yamezidi kufanya mashambulio ya anga katika eneo la bandari ya mafuta linaloshikiliwa na waasi Ras Lanuf, katika mapigano mapya.

Walioshuhudia walisema ndege za kivita zimeangusha makombora katika maeneo waishio watu na karibu na maeneo waishio waasi.

Hapakuwa na taarifa zozote za mauaji.

Wakati huo huo, msemaji wa waasi alisema mwakilishi wa Kanali Gaddafi alipendekeza kufanya mazungumzo atakapoondoka.

Msemaji huyo alisema, waasi hao walikataa pendekezo hilo.

Mtu mmoja wa upinzani, Jalal al-Gallal, aliiambia BBC: "Kuondoka ni jambo moja, lakini kutoshtakiwa baadae haikubaliki."

'Udhibiti wa kijeshi'
Hakujakuwa na kauli yeyote kutoka serikali ya Kanali Gaddafi kutokana na kauli hiyo ya waasi, lakini kiongozi huyo wa Libya amekataa kuachia madaraka enzi za nyuma.

Anadai hana nafasi yeyote, na hivyo haiwezekani kwake kujiuzulu.

Mwandishi wa BBC Wyre Davies, mjini Tripoli, alisema upande wa Kanali Gaddafi unaamini unazidi kuhodhi eneo kubwa kijeshi, wakidhibiti eneo la magharibi mwa Libya.

Siku ya Jumatatu, majeshi yanayomwuunga mkono Kanali Gaddafi yalidhibiti upya mji wa Bin Jawad, kwenye barabara inayoelekea Ras Lanuf, eneo lililohodhiwa na waasi siku ya Ijumaa.

Kwa kushambulia kwa njia ya anga, helikopta na silaha nzito, waliweza kuwasukuma waasi katika pwani ya kaskazini.

Mwandishi wetu alisema kwa hali hii, ni vigumu kuona uongozi wa Gaddafi ukitaka kuzungumzia suala la kurithiwa.











Bunge la Hungary jana usiku limepiga kura kuyapitisha marekebisho ya sheria ya vyombo vya habari na kukubaliana na matakwa ya Umoja wa Ulaya.

Sheria ya hapo kabla ambayo ilianza kutumika mwanzoni mwa mwaka huu, ilionekana na baadhi, ikiwemo kamisheni ya Umoja wa Ulaya, kuwa ni ukandamizaji wa uhuru wa habari.

Marekebisho hayo mapya yanaondoa vifungu vya sheria ambavyo vilikuwa vinataka vyombo vya habari, kama vile mtandao wa internet na blog, kutoa habari zisizoegemea upande mmoja, na kwamba shughuli zote za vyombo vya habari ni lazima zisajiliwe serikalini. Aidha marufuku dhidi ya habari zinazochukuiliwa kuwa ni za uchokozi imeondolewa.

Wimbi la upinzani kutoka jumuiya ya kimataifa dhidi ya sheria hiyo limeigubika nafasi ya Hungary ya kiti cha urais wa Umoja wa Ulaya ambacho huzunguka miongoni mwa nchi wanachama kila baada ya miezi sita



The Hungarian Parliament Building (Hungarian: Országház)


Parliament Building



The Hungarian Parliament Building (Hungarian: Országház) is the seat of the National Assembly of Hungary, one of the Europe's oldest legislative buildings, a notable landmark of Hungary and a popular tourist destination of Budapest. It lies in Kossuth Lajos Square, on the bank of the Danube, in Budapest.

History


Budapest was united from three cities in 1873 and seven years later the National Assembly resolved to establish a new, representative Parliament Building, expressing the sovereignty of the nation. A competition was published, which was won by Imre Steindl, but the plans of the other two competitors were also realized, facing the Parliament: one serves today as the Ethnographical Museum, the other as the Ministry of Agriculture









Rais Obama atengua sheria marufuku ya kesi za ugaidi





Rais Barack Obama wa Marekani ameondoa marufuku ya miaka miwili dhidi ya kesi mpya za wafungwa wa jela la Guantanamo Bay, na hivyo kurejesha mahakama ya kijeshi dhidi ya watu hao iliyoanzishwa mwaka 2006 na mtangulizi wake, George Bush.

Mwaka 2009 Rais Obama kwa mara ya kwanza alipokuwa rais, alisitisha mashtaka mapya dhidi ya watu wanaoshikiliwa katika jela hilo na kuamrisha kupitiwa upya kwa sheria za kuwaweka watu kizuizini na kuahidi kulifunga jela hilo katika kipindi cha mwaka mmoja.

Hata hivyo, alishindwa kutekeleza ahadi hiyo, na kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wabunge wa nchi yake ambao wamekuwa wakipinga kusikilizwa kesi za washukiwa wa ugaidi katika mahakama za kiraia nchini Marekani.

Wakati ambapo Rais Obama alitaka baadhi ya washukiwa hao wa ugaidi washtakiwe katika mahakama za Marekani, maelekezo yake hayo mapya pia yaanazisha utaratibu wa kuwashikilia washukiwa bila ya kuwashtaki kwa muda usiojulikana.






Rais wa zamani wa Ufaransa kupanda kizimbani leo




Rais wa zamani wa Ufaransa, Jacques Chirac, leo anatarajiwa kupanda kizimbani katika siku ya pili ya kesi ya rushwa inayomkabili.

Rais huyo wa zamani wa Ufaransa anakabiliwa na makosa ya ubadhirifu wa fedha za umma wakati alipokuwa meya wa jiji la Paris katika kipindi cha miaka ya 1990 kabla ya kuwa rais wa nchi hiyo.

Inadaiwa kuwa ajira bandia zilianzishwa ili kupata fedha ambazo bwana Chirac aliwapatia marafiki zake. Rais huyo wa zamani alikuwa na kinga ya kutoshtakiwa wakati alipokuwa rais katika kipindi cha kuanzia mwaka 1995 hadi 2007, na mara zote amekuwa akikanusha mashtaka hayo.

Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa Ufaransa kupandishwa kizimbani katika historia ya nchi hiyo.







Loriondo hakutoshi! watu wamiminika kufata dawa ya Ukimwi



KUFUATIA kujitokeza kwa Mchungaji Mbilikile Masakile kutangaza kutibia magonjwa sugu kupata dawa aliyooteshwa na Mwenyezi Mungu, watu wamezidi kumiminika Wilayani Loriondo mkoani Arusha kufuata dawa hiyo.
Mchungaji Mbilikile alijitokeza na kutangaza kuwa na dawa ya kutibia magonjwa yakiwemo ya Ukimwi, Tb, Presha na mengineyo, dawa ambayo alidai kuoteshwa na Mwenyezi Mungu.

Mchungaji Mbilikile anatoa tiba hiyo katika kijiji cha Samunge Kata ya Digodigo Wilayani Loriondo mkoani Arusha kwa kuchemsha mizizi hiyo na kuwapa dawa hiyo papohapo na mara utumiapo dawa hiyo mgonjwa hupona papohapo imedaiwa.

Dawa ya Mchungaji huyo hupatikana kwa sharti ya kunywa papohapo na hairuhusiwi kuondoka nayo na tiba hiyo hutoa kwa kiasi cha shilingi mia tano ya kitanzania 500/= tu.

Imedaiwa na mashuhuda waliofika eneo hilo kuwa mchungaji huyo huchemsha mizizi hiyo ya mti aliougundua kwa kuoteshwa na Mungu uliopo katika kijiji hicho na mara amalizapo kuchemsha dawa hiyo huiombea dawa hiyo na kuwapa wagonjwa papohapo.

Watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo viongozi kutoka sehemu tofauti wamekuwa wakimiminika kufata dawa hiyo inayotibu maradhi hayo sugu.

Baadhi ya wagonjwa ambao tayari wamekunywa dawa hiyo wamedai kupona maradhi ambayo yamekuwa yakiwasumbua na mmoja hata kuthubutu kuithibitishia NIFAHAMISHE kuwa amepona ukimwi kwa kuwa alipotoka kunywa dawa hiyo alipokwenda kufanya vipimo alionekana hana virusi hivyo alibainisha kwa sharti la kutotajwa jina.

Kufuatia uwingi wa watu kijijini hapo alipo mchungaji huyo kuna wasiwasi wa kutokea maradhi ya mlipuko kutokana na kuwa watu kujisaidia hovyo kwenye majani kwa kukosekana huduma ya choo mahali hapo.

Kufuatia hali hiyo Serikali imesitisha safari za kwenda Loriondo kutokana na mlundikano wa watu na magari eneo hilo na usalama kuwa mdogo kutokana na mlundikano huo kwa kuwa hivi sasa watu wamekuwa wakishindwa kwenda na kurudi kutokana na watu kuwa wengi tofauti na awali ukifika unakumnywa dawa na kurudi siku hiyo hiyo.

Nauli nayo imepanda maradufu kutokana na waendeshaji wa usafiri kuona biashara imenona na hivi sasa nauli imepanda na kufikia shilingi laki moja na elfu ishirini kutoka Arusha mjini hadi kwenda Wilayani Loriondo.

Kwa habari zaidi juu ya mchungaji huyu itazidi kuwajia hapahapa kadri uchunguzi wa dawa hii utakavyofanyika







Vijana kuandamana Kuwait




Wimbi la maandamano ya upinzani katika mataifa ya kiarabu linazidi kusambaa, ambapo leo hii makundi ya vijana nchini Kuwait yamepanga kuandamana.







Makundi hayo yamepanga kuandamana bila ya kibali cha serikali, hali inayoyafanya maandamano yao kuwa haramu. Waandamanaji hao wanataka uhuru zaidi wa kisiasa pamoja na kuondoka madarakani kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Kuwait imekuwa ikitawaaliwa na watu wa kutoka familia moja kwa kiasi cha miaka 250 sasa.








Kesi ya ufisadi ya Bw Muluzi yaanza




Rais Bingu wa Mutharika
Kesi ya aliyekuwa Rais wa Malawi Bakili Muluzi imeanza akituhumiwa kwa mashtaka ya ufisadi.

Mahakama Kuu ilikataa ombi lililotolewa Jumatatu kuzuia kesi hiyo kwa misingi ya hali ya afya ya Bw Muluzi.

Aliyekuwa Rais huyo ametuhumiwa kwa matumizi mabaya ya takriban dola za kimarekani milioni 11 zilizotoka kwa wafadhili wa kimataifa.

Amekana mashtaka hayo- na mara zote amekuwa akisema hayo yote yametokea kutokana na kutofahamiana na Bingu wa Mutharika ambaye alikuja kuwa Rais mwaka 2004 baada ya yeye kumaliza muda wake.

Bw Muluzi alikamatwa mwaka 2005 kwa madai ya kuhusika na ufisadi, lakini hivi karibuni kesi hiyo imekuwa ikicheleweshwa kutokana na afya yake.

Mwandishi wa BBC Raphael Tenthani aliyopo Blantyre alisema tangu ajiuzulu mwaka 2004, Bw Muluzi amefanyiwa upasuaji wa mgongo mara kwa mara.

Rais Mutahrika alikwaruzana na Bw Muluzi baada ya kuingia madarakani, na kumshutumu mwenziwe ambaye aliwahi kumwuunga mkono kwa kuharibu mpango wake wa kupambana na ufisadi.









‘Fulana nyekundu iliniponza’



KIJANA aliyejeruhiwa juzi na Simba huko Mbagala Kuzuiani amebainisha kuwa aliponzwa na fulana nyekundu aliyokuwa amevaa siku hiyo ya tukio.


Akiongea akiwa wodini katika taasisi ya MOI Muhimbili alidai kuwa ameponzwa na fulana nyekundu aliyokuwa amevaa kwa kuwa Simba huyo alikuwa akimkimbiza syeye tu katika kundi lote la watu waliofika kumshuhudia.

Alidai siku hiyo alikuwa ni miongoni mwa watu waliofika kumshuhudia lakini ghafla aliweza kurukiwa na Simba huyo na alipokuwa akijaribu kujihami na kukimbia katika kudni la watu sima huyo alizidi kumfata yeye.

Alidai alijihami kwa kukimbilia na kupanda katika mti wa mnazi lakini bado simba huyo alimfata na kumparura kwa kumshika sehemu zake za shingoni na aliweza kuachiwa na simba huyo baada ya kusikia kelele za watu na kukimbia nay eye kukimbizwa hospitali








Majeshi ya Gaddafi yawazingira waasi




Wasiwasi umezidi kuongezeka wa kuzuka janga la kibinaadamu mnamo wakati ambapo majeshi yanayomuunga mkono kiongozi wa Libya Kanali Mohammar Gaddafi yameizingira miji ya Misrata na Zawaiya ambayo ni ngome ya waasi nchini humo.
Ishara zinaonesha kuwa Kanali Gaddafi amedhamiria kupambana na uasi huo kwa nguvu zote.

Ufaransa na Uingereza zinalichagiza Baraza la Usalama la Umoja wa Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kuzuia ndege kutoruka juu ya anga ya Libya. Maafisa wa Marekani, kwa upande wao, wamekuwa wakisita kukubaliana na azimio hilo.




Hata hivyo, Rais Barack Obama, kwa mara ya kwanza, amezungumzia uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi kuumaliza mzozo huo nchini Libya au kushawishi mkondo wa mambo utakavokwenda.


Wakati huo huo, katibu Mkuu wa Umoja wa kujihami wa mataifa ya Magharibi, NATO, Anders Fogh Rasmussen amewaambia waandishi wa habari vile ambavyo anashangazwa na jumuiya ya kimataifa kumuangalia Kanali Gaddafi akiwaua raia wake.

Umoja wa Mataifa umeteua mjumbe maalum kuchunguza maafa yaliyowakuta watu nchini Libya, na umetoa wito wa kupatikana kiasi cha dola millioni 160 kwa ajili ya kufadhili makaazi, chakula na maji safi na vyoo kwa ajili ya wakimbizi wanaojaribu kukimbia kutoka Libya










Siku ya akinamama ulimwenguni





Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Wanafunzi waadhimisha siku ya akinamamaAkinamama waadhimisha miaka 100 tangu walipoanzisha juhudi za kudai haki sawa na wenzao wa kiume.Jee juhudi hizo zimeleta matunda yanayotarajiwa?

Siku ya wanawake ulimwenguni imeanza kuadhimishwa tangu miaka 100 iliyopita nchini Denmark,Ujerumani,Austria,Uswisi,Bulgaria na Marekani. Wakati ule akinamama zaidi ya milioni moja waliteremka majiani kudai haki yao ya kimsingi- haki ya kupiga kura.

Hebu fikiria, miaka mia moja iliyopita wanawake hawakuwa hata na haki ya kupiga kura katika nchi nyingi za dunia. Hii leo, siku ya akinamama inaadhimishwa kwa kutathmini maendeleo yaliyoweza kupatikana tangu wakati huo, na kuzingatia changamoto zinazowakabili wanawake katika kila pembe ya dunia.

Nchini Ujerumani siku ya akinamama iliyopewa jina na mtandao wa akinamama wa Berlin- "Miaka mia moja ya subira- miaka 100 ya ghadhabu" inaadhimishwa kwa namna mbali mbali. Licha ya baadhi ya ufanisi, bado hali inadhibitiwa na wanaume- na hasa linapohusika suala la ajira, wanalalamika wanamtandao. Idadi kubwa zaidi ya akinamama katika daraja za uongozi ikilazimika itengwe idadi na kuwarahisishia akinamama njia za kuweza kufungamanisha kazi na familia. Hilo ni dai la mawaziri wa kike wa serikali kuu.

Bibi Jutta Wagner, mwenyekiti wa shirikisho la wanasheria wa Ujerumani, anahisi maendeleo yaliyofikiwa ni haba:





Haki sawa kwa wote
"Maendeleo ni haba mno kuweza kusema kwamba pengine mwaka 2090 idadi kubwa zaidi ya wakinamama watakauwa wanashikilia nyadhifa za juu za uongozi". Hali hiyo, itabadilika tu ikiwa kweli sheria maalum zitatumika- hivyo ndivyo tunavyoamini hasa kutokana na uchunguzi tulioufanya- imani yetu ni kubwa kuliko wakati wowote ule mwengine.

Marekani siku ya kimataifa ya akinamama inapita bila ya harakati zozote zile, licha ya kwamba bunge limeitambua rasmi siku hiyo tangu mwaka 1994. Hata hivyo, dai kuu la vuguvugu la akinamama nchini humo ni kuona kifungu kinachohusiana na haki sawa kati ya jinsia kinaingizwa katika katiba.

Katika ulimwengu wa kiarabu haijulikani bado kama wimbi la mageuzi linalopiga hivi sasa litabadilisha pia hali ya akinamama katika nchi hizo. Katika wakati ambapo nchini Syria akinamama wanaruhusiwa kufanya kazi bega kwa bega na wenzao wa kiume, nchini Saudi Arabia, kwa mfano, ndio kwanza akinamama wanadai haki ya kuruhusiwa kuendesha gari.





Mauwa kwa wakainamama
Barani Afrika, tunachukua mfano wa Kenya, ambako ingawa siku ya kimataifa ya akinamama si siku ya mapumziko, hata hivyo, jumuiya ya wanawake na maendeleo-jumuiya kubwa yenye wanachama zaidi ya milioni nne na nusu, inawazindua akinamama mnamo siku hii ya leo wawajibike zaidi, hasa kwa kuzingatia uchaguzi wa mwakani pamoja na kushadidia mshikamano pamoja na dada zao katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.







Baba atesa mtoto kwa kumpa adhabu kali –Arusha




MTOTO Jerry Martin [5] amelazwa katika hospitali ya MountMeru kutokana na majeraha aliyoyapata kutokana na adhabu na mateso aliyoyapata kutoka kwa baba yake mzazi.
Jerry amekuwa akiteseka kwa muda mrefu kwa kupata adhabu kali kutoka kwa baba yake mzazi aliyetambulika kwa jina la Lema na kumsababishia majeraha makali maeneo yake ya mwili.

Bw. Lema amekuwa akimtesa mtoto huyo kwa kile alichodai mwanae huyo amekuwa hajui kusoma wala kuandika na amekuwa akimuadhibu mara kwa mara kutokana na sababu hiyo aliyoidai.

Imedaiwa kuwa Lema amekuwa akimuadhibu mtoto huyo kwa lengo la kumuua ili aweze kuoa mwanamke mwingine baada ya mama wa mtoto huyo kufariki dunia.

Imedaiwa kuwa, Lema amekuwa akipata shinikizo kutoka kwa wanawake anaotaka kuwaoa kuwa hawataweza kulea mtoto wa kambo hivyo amekuwa akifanya hivyo ili mtoto huyo aweze kupoteza maisha ili aweze kuoa.

Bw. Lema amekuwa akimuadhibu mtoto huyo kwa kumpa kipigo cha nguvu na hatimaye kumuunguza sehemu zake za mwili na wakati alipokuwa akifanya hivyo alikuwa akimfungia chumbani na kumziba mdomo ili sauti isiweze kusikika nje ya nyumba hiyo.

Pia alikuwa akimlaza mtoto huyo nje ya nyumba mara kwa mara na kuthubutu kumnyima chakula .

Na alimsihi mtoto huyo asitoe siri hiyo kwa majirani na watu wengine na akimbaini kuwa anatoa siri hiyo ya kumuadhibu alimuhidi kumtoa uhai wake.

Hata hivyo mateso ya mtoto huyo yaligundulika na mwalimu wake wa shule ya awali kwa kumuona mtoto huyo akiwa dhofu na kusikia harufu kali ya vidonda vilivyotunga usaha yanayotoa harufu na ndipo alipomchunguza alibaini majeraha makali na ndipo papohapo alipokwenda kutoa ripoti katika kituo cha polisi cha Ngarinalo Arusha.

Mtoto huyo amegundulika majeraha makubwa sehemu zake za makalio kuungua vibaya, maeneo yake ya kifua, mkono wake wa kushoto na imesemekana karibia mwili mzima ulikuwa na majeraha makubwa yaliyovilia usaha na kutoa harufu kali.

Mtoto huyo alibainisha kuwa alikuwa akipata adhabu hizo mara nyingine kwa kupigwa na hata kuunguza na moto.

Kutokana na hali ya mtoto huyo watu waliomuona wakati akikaguliwa waliweza kuangua vilio na hata askari polisi nao waliweza kutoa machozi kutokana na hali ya mtoto huyo.

Asubuhi hii imedaiwa kuwa hali ya mtoto huyo imedaiwa kuwa ni mbaya na bado anaendelea na matibabu hospitalini hapo.

Kufuatia hali hiyo Lema anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo








Gbagbo sasa adhibiti mauzo ya Kakao








Gbagbo sasa adhibiti mauzo ya Kakao

Wadadisi wanasema utawala wa Gbagbo hauna pesa za kunua kakao kutoka wakulima
Laurent Gbago ameamuru kuwa serikali yake isimamie mauzo yote ya zao la kakao nchini Ivory Coast na kwenye soko za kimataifa.

Gbagbo ametangaza kauli hiyo kwenye televisheni ya kitaifa, ambapo alisema utawala wake sasa utanunua zao hilo kutoka wakulima wote nchini humo.




Tangazo hili litabdadilisha sana mauzo ya zao kakao. Serikali ndio itakayo nunua zao hilo kutoka kwa wakulima laki saba kote nchini humo, tofauti na mfumo wa soko huru uliopo sasa.


Kwanzia sasa serikali itaamua bei kila msimu wa mavuno. Wadadisi wanasema tangazo hili litavuruga soko la zao hilo na kutakuwepo na faida kidogo sana kwa utawala wa Gbagbo ambao unataka kudhibiti biashara hiyo muhimu.


Hapo awali, Alassane Ouatarra anayetambulika na jumuiya ya kimataifa kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi wa urais nchini humo, alitaka biashara ya kakao isusiwe kwa muda kama njia moja ya kumshinikiza Gbagbo aondoke mamlakani. Kakao inatumika kutengeneza chokoleti, kiburudisho muhimu duniani na Ivory Coast ndio nchi ya tatu duniani kwa kuzalisha zao hilo.




Hata hivyo vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa ulaya vitatatiza sana mauzo ya zao hilo katika nchi za ulaya, ambazo ni soko muhimu la kakao kutoka Ivory Coast.

Mwandishi wa BBC mjini Abidjan, anasema itakuwa vigumu kwa utawala wa Gbagbo kutekeleza amri hii kwa kuwa haina fedha za kuwalipa wakulima, takwimu za wanaozalisha zao hilo na hata ghala za kuhifadhi kakao zitakazo vunwa. Anasema tangazo hilo litachochea zaidi biashara ya magendo kupitia nchi jirani kama vile, Ghana, Togo na Liberia.






'Video ya Misri' Wazimbabwe 38 waachiwa




Polisi wakiwalinda waliotiwa mbaron, Harare
Wazimbabwe 38 waliokamatwa mwezi uliopita kwa kujadili ghasia zilizofanyika Misri wameachiwa huru lakini wanane wamebaki rumande.

Walikamatwa Februari 19 baada ya kuhudhuria mhadhara na kutazama video za ghasia hizo zilizofanyika Misri zilizomwondoa kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu Hosni Mubarak.

Miongoni mwa walio bado mbaroni ni aliyekuwa mbunge wa upinzani Munyaradzi Gwisai, anayetuhumiwa kuhusika katika kuandaa mkutano huo.

Wanaweza kukabiliwa na mashtaka ya uhaini, ambapo unaweza kupata hukumu ya kifo.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamelaani hatua ya kuwakamata watu hao.

Wakili wa utetezi Alec Muchadehama alisema serikali imefuta mashatka dhidi ya watu hao 38 kutokana na kukosa ushahidi.

Alisema waliokamatwa walikuwa wakishiriki katika majadiliano ya kitaaluma juu ya siasa za Afrika.

Baadhi walisema waliteswa walipokuwa kizuizini.

Lakini waendesha mashtaka wanawatuhumu kwa kujadili namna ya kuiondosha serikali iliyopo kwa mujibu wa katiba










BIN JAWWAD, Libya — Forces loyal to Moammar Gadhafi, some in helicopter gunships, pounded opposition fighters with artillery, rockets and gunfire Sunday, dramatically escalating their counteroffensive to halt the rebels' rapid advance toward the capital.

They also battled to loosen the grip of rebels on two cities close to Tripoli. But in at least one case, their tactics appeared to lead them into a trap.

Residents said pro-Gadhafi troops punched into the city of Misrata, 120 miles (200 kilometers) east of Tripoli, the capital, with mortars and tanks but were pushed out five hours later by rebel forces. The rebel commanders intentionally opened the way for government tanks to enter the city, then surrounded them and attacked with anti-aircraft guns and mortars, said Abdel Fatah al-Misrati, one of the rebels.




"Our spirits are high," al-Misrati said. "The regime is struggling and what is happening is a desperate attempt to survive and crush the opposition. But the rebels are in control of the city."

As fighting across Libya grew more fierce, the international community appeared to be struggling to put military muscle behind its demands for Gadhafi to give up power.

A small British delegation sent to talk to the rebels headquartered in the main eastern city of Benghazi, meanwhile, was arrested by the rebels themselves, who said the group had entered the country without permission. The rebels have set up an interim governing council that is urging international airstrikes on Gadhafi's strongholds and forces, though they strongly oppose foreign intervention on the ground.

Sunday's fighting appeared to signal the start of a new phase in the conflict, with Gadhafi's regime unleashing its air power on the rebel force trying to oust the ruler of 41 years. Resorting to heavy use of air attacks signaled the regime's concern that it needed to check the advance of the rebel force toward the city of Sirte — Gadhafi's hometown and stronghold.

Advertise | AdChoicesAdvertise | AdChoices
Advertise | AdChoices
.Anti-Gadhafi forces would get a massive morale boost if they captured Sirte, and it would clear a major obstacle on the march toward the gates of Tripoli.

The uprising against Gadhafi, which began Feb. 15, is already longer and much bloodier than the relatively quick revolts that overthrew the longtime authoritarian leaders of neighboring Egypt and Tunisia.

Libya appears to be sliding toward a civil war that could drag out for weeks, or even months. Both sides seem to be relatively weak and poorly trained, though Gadhafi's forces have the advantage in numbers and equipment.

The conflict took a turn late last week when government opponents, backed by mutinous army units and armed with weaponry seized from storehouses, went on the offensive. At the same time, pro-Gadhafi forces have conducted counteroffensives to try to retake the towns and oil ports the rebels have captured since they moved out of the rebel-held east.

An opposition force estimated at 500 to 1,000 fighters pushed out of the rebel-held eastern half of Libya and has been cutting a path west toward Tripoli. On the way, they secured control of two important oil ports at Brega and Ras Lanouf.

If the rebels continue to advance, even slowly, Gadhafi's heavy dependence on air power could prompt the West to try to hurriedly enforce a no-fly zone over the country. The U.N. has already imposed sanctions against Libya, and the U.S. has moved military forces closer to its shores to back up its demand that Gadhafi step down



Africans say Libyan troops try to make them fight








Libyan troops loyal to Muammar Gaddafi are rounding up black African migrants to force them to fight anti-Gaddafi rebels, said young African men who fled to Tunisia.

In separate accounts at this refugee camp, they said they were raided in their homes by soldiers, beaten and robbed of their savings and identity papers, then detained and finally offered money to take up arms for the state.

Those who refused were told they would never leave, said Fergo Fevomoye, a 23-year-old who crossed the border on Sunday, Reuters reports.

"They will give you a gun and train you like a soldier. Then you fight the war of Libya. As I am talking to you now there is many blacks in training who say they are going to fight this war. They have prized (paid) them with lots of money.

He said Africans who are first intimidated and stripped of everything were then offered 250 Libyan dinars to train as fighters.

"They said I should take money and fight. They would give me 250 dinars. I said No. When I told them No they told me I would not go anywhere," he told Reuters.

The Libyan governemnt has denied using foreign nationals to fight the rebels, saying instead that dark-skinned Libyans serving in its security forces had been mistaken for African mercenaries.

INSTANT "MERCENARIES"
When protests against Gaddafi's government led to violence three weeks ago, rebels spread reports that the Libyan leader had brought in African mercenaries from such states as Chad and Zimbabwe.

But the suggestion that trained, uniformed troops were being flown in to help suppress the revolt has not been proven.

The accounts now emerging of how some black migrants are successfully being forced into taking up arms for the Libyan state may be one explanation of these reports of black fighters.
Whatever the truth, Nigerian and Ghanians in this transit camp all say they were suddenly very afraid to show their faces in the cities of western Libya where they worked, in case they were taken for mercenaries or dragooned by government troops.

Obinna Obielu, an electrician who had worked in Libya for 12 years and said he had saved 10,000 dollars, escaped with his two friends and their wives and two babies in an old Land Cruiser.

Obielu said the main road from Zawiyah, 50 km (30 miles) west of Tripoli was too dangerous, and he had driven through the bush close to the frontier.
"I go off, because it is not a good road. Because they are attacking people and sending them back to go and fight in the war," he said. "The car is left back there."

Daniel Chibuzor and Tijanx Sadiki also recounted how they were raided and robbed at home and left with no papers and no money for food, terrified of appearing on the streets, before they decided to risk travelling west to Tunisia.

A baby daughter, Ability, and infant son, Miracle, travelled with the group. Ability needed treatment at the Tunisian Army's mobile hospital for tear-gas inhalation.
Nigerian Ike Emanuel, who made it to the safety of Tunisian territory last week after burying his six-month-old baby in the desert, said he had talked to many of the latest arrivals among his countrymen and heard the same theme: Africans were being trapped and forced to either fight or flee.

Over 105,000 migrant workers have fled from Libya into Tunisia in the past 10 days, most of them Egyptians but also including some 20,000 Bangladeshis. The Egyptians have since been reptriated by airlift, after making angry protests about the Cairo government's alleged inaction.
The Bangladeshis and thousands of west Africans remain in the United Nations refugee agency's transit camp, which is being prepared for a possible influx of refugees the agency fears may be trapped inside Libya but desperate to escape.

Fergo Fevomoye said it was a sympathetic Libyan policeman who eventually helped him escape, "because if not I am going to stay here 20 years, I am going to die here

No comments:

Post a Comment