KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, March 10, 2011

Jerry na wenzake wana kesi ya kujibu


MSHITRAKIWA wa kwanza katika kesi ya kuomba rushwa ya Shilingi Milion 10 Jerry Muro na wenzake wameonekana wna kesi ya kujibu .
Muro na wenzake wanadaiwa kuomba rushwa hiyo kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, Michael Wage.


Hakimu Gabriel Mirumbe aliyasema hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kusikiliza ushahidi wa upande wa Serikali na kubaini kuwa washitakiwa wote wana kesi ya kujibu.


Muro na wenzake Edmund Kapama na Deogratius Mgasa wote kwa pamoja wanadaiwa kudai na kutaka kupokea rushwa ya Shilingi milioni 10 kutoka kwa Wage rushwa waliyokiuwa wakiidai kinguvu kwa kutumia vitisho.


Kesi hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa Machi 29 mwaka huu










Masharti ya dawa hiyo ni hizi hapa



DAWA inayotolewa na mchungaji Ambilikile inauwezo wa kutibu magonjwa sugu yaliyoshindikana yakiwemo Ukimwi, Kisukari,Kifua, Presha na mengine mengi na watu wamethibitisha kupona baada ya kunywa dawa hiyo.
Dawa hiyo hutolewa na yeye mwenyewe ambao huichemsha na akimaliza hufanya sala fupi ya kuiombea na kisha kugawa kwa wagonjwa kwenye kikombe na kunywa.

Sharti ya dawa hiyo ni kupewa moja kwa moja na mkono wa mchungaji huyo vinginevyo dawa hiyo haitaweza kufanya kazi pindi uinywapo.
Sharti lingine dawa hiyo hutakiwa kunywa hapohapo alipo na hata ukichukua kipande cha mti wa dawa hiyo na kuondoka nao kuuchemsha nyumbani kwako pia haitafanya kazi

Sharti jingine dawa hiyo hutakiwa kulipia kiasi cha shilingi mita tano tu na haruhusu kuzidisha hata kama mgonjwa akimpa hela ya ziada, imedaiwa kuwa mchungaji huyo hukataa hela anazopewa na wagonjwa hao na kuwambia ni bora wamnunulie zawadi wamletee lakini si kumpa pesa zaidi ya alichopangiwa na Mwenyezi Mungu.

Wakati huohuo Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), limesema linatambua na kubariki dawa inayotolewa na Mchungaji wake mstaafu anayefanyia shughuli zake Loliondo, Ambilikile Mwasapile, huku baadhi ya maaskofu wa kanisa hilo wakithibitisha kwamba wamekunywa dawa hiyo na kuponywa










Ambilikile aonya wafanyabiashara




MCHUNGAJI MSTAAFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Mbilikile Masakile [78] amewatisha wafanyabiashara wote wanaopandisha kiholela nauli na huduma muhimu kwa lengo la kujinufaisha katika fursa hiyo ya matibabu kuwa hawatafika mbali watafilisika.
Mchungaji huyo amekemea hivyo baada ya kuzuka kwa wimbi la wafanyabiashara na kulangua na kupandisha nauli kila kukicha kwenda wilayani Loriondo anakotoa huduma ya uponyaji.

Mchungaji huyo amesema wale wote wanaopandisha nauli kwa ajili ya kujinufaisha isivyo halali watafilisika muda si mrefu na kuwapa onyo kali wasiendelee kufanya hivyo.

Mbali na wanaopandisha nauli pia aliwataka wale wote wanaotoa huduma muhimu katika kijiji hicho yakiwemo maji na vyakula katika kijiji hicho kuacha kupandisha bei maradufu kwa lengo la kujitajirisha.

Walanguzi hao wamefikia kuuza maji ya chupa ya nusu lita iliyokuwa ikuuzwa kwa shilingi 500 sasa inauzwa kwa shilingi 1500, maji ya lita moja yaliyokuwa yakiuzwa kwa shilingi 1000 yamefikia kuuzwa shilingi 2500 na chakula kilichokuwa kikiuzwa sahani shilingi 1000 kimefikia kuuzwa shilingi 2500 hii imetokana na walanguzi hao kuona watu kufurika eneo hilo.

Awali nauli kutoka Arusha Mjini kwenda wilayani humo kabla mchungaji huyo hajajitokeza ilikuwa shilingi 35,000 na baadae ilifika 50,000/= na sasa imepanda kutoka huko na kufikia shilingi 120,000/=

Hata hivyo watu wamekuwa wakikubaliana na hali halisi ya nauli hiyo ili waweze kumfikia mchungaji huyo kunywa dawa hiyo waweze kupona maradhi yao.

Imedaiwa asubuhi hii zaidi ya watu elfu kumi wapo kijijini hapo wakisubiri kunywa dawa hiyo






Vigogo wavuruga utaratibu Loriondo




WATU wanaosadikiwa kuwa ni vigogo wa serikali waliofika kunywa dawa ya mchungaji Ambilikile wamevuruga utaratibu mzima wa foleni uliowekwa katika kupata dawa hiyo.
Vigogo hao wamedaiwa kuvuruga utaratibu wa foleni na kutumia madaraka yao vibaya kutaka wapatiwe huduma hiyo kabla ya watu wengine waliowakuta mahali hapo.

Hivyo kutokana na tabia hiyo inayofanywa na viongozi hao, watu wameamua kufanya fujo na kuvamia jiko linalochemshiwa dawa hiyo na kuanza kunywa dawa hiyo huku wakipinga vurugu inayofanywa na viongozi hao.

Kufuatia hayo wagonjwa zaidi ya sita wamefariki dunia kabla hawajamfikia mchungaji huyo kutokana na kuzidiwa kwa maradhi na kuwa na uwingi wa watu na kusababisha foleni kubwa kumfikia mchungaji huyo.

Wagonjwa 3000 humfikia mchungaji huyo kupata huduma hiyo kila siku kwa uataratibu uliowekwa hapo.

Kufuatia ubora wa dawa hiyo uliothibitishwa na wagonjwa na viongozi waliokunywa kukiri kupona magonjwa yao yaliyokuwa yakiwasumbua, wagonjwa wengi wamekuwa wakitoka hospitalini huku wengine wakitoroshwa na ndugu zao na kukimbilia wilayani Loriondo kunywa dawa hiyo.

Katika uchunguzi wa NIFAHAMISHE baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakiomba ruhusa za kufiwa huku wengine kudai wanauguliwa ili wapate fursa ya kwenda huko baada ya dwa hiyo kuthibishwa na wagonjwa hao.

Pia idadi kubwa imepungua katika makanisa wale wanaofika katika huduma za maombezi kuombewa matatizo na maradhi yanayowakabili na kukimbilia mkoani Arusha.

Magari yanayokwenda kuelekea kwa mchungaji huyo katika kata ya Digodigo, katika kijiji cha Samunge huko wilayani Loriondo msururu wa magari wafikia kilomita ishirini kuelekea huko.

Kutokana na hilo serikali imeongeza askari polisi eneo hilo kulinda usalama eneo hilo ikiwemo na kuongeza askari wakuongoza magari barabarani kuanzia Arusha Mjini kuelekea Loriondo






Usalama I Coast wazidi kuwa na utata



Vijana wanaomwuunga mkono Ouattara
Raia wa Ivory Coast wanashuhudia ongezeko la silaha na mapanga kwenye mitaa ya mji wao mkuu, jambo ambalo limewatia wasiwasi wa nchi yao kuweza kurejea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kwa zaidi ya miaka minane nchi hiyo imegawika baina ya kaskazini, eneo linalotawaliwa na waasi na kusini ambako serikali inatawala.

Inaaminika kuwa jeshi lenyewe limegawanyika na habari za kuaminika zinasema kuwa wengi wa wanajeshi hao walimpigia kura Bw Ouattara.

Magharibi ya mbali ya nchi, vikosi vinavyomuunga mkono Bw Ouattara kutoka kaskazini mwa nchi vimeteka miji mitatu iliyo kwenye mpaka wa Liberia katika hatua inayoaminika kuwa ya kuzuia maharamia wasiingie nchini humo.

Lakini mbali na kutishia maeneo mbalimbali waasi wamesita kufanya shambulio kubwa la kuelekea kusini wakidai kuwa wanaheshimu mikataba ya amani - ambayo inaweza kubadili hali ya mazungumzo ya amani yanayoendelea na Umoja wa Afrika.

Labda wasiwasi mkubwa kwa Laurent Gbagbo ni ghasia zilizojitokeza mjini Abidjan, ambako sehemu kubwa ya wilaya ya Agogo imekuwa hatari hata kwa vikosi vya usalama.

Kambi ya Ouattara bado ina matumaini ya msaada wa kijeshi kutoka nje ya nchi labda kwa njia ya vikosi vya kimkoa kutoka shirikisho la ECOWAS.

Umoja wa Mataifa una takriban askari 10,000 wa kulinda amani ambao hadi sasa wameshindwa kuzuia machafuko.

No comments:

Post a Comment