KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Monday, March 7, 2011
Magari Saba Ya Kifahari Kwaajili ya Wake wa Rais
Pamoja na kwamba ana ndege yake maalumu ya kiraisi na msururu wa magari ya serikali anayoambatana nayo katika misafara yake, rais Jacob Zuma anatafuta magari saba ya kifahari kwaajili ya wake zake.
Kamati ya ulinzi wa rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma imetangaza kutoa tenda ya kukodisha magari saba ya kifahari kwaajili ya wake wa rais Zuma .
Katika miji saba ya Afrika Kusini ukiwemo mji anaotoka Jacob Zuma wa KwaZulu-Natal kutakuwepo na gari moja ambalo litakuwa tayari tayari kwaajili ya wake wa Rais Zuma.
Kwa mujibu wa nyaraka za tenda ya kukodisha magari hayo, magari yanayohitajika yanatakiwa yawe ni magari mapya ya kifahari na magari hayo lazima yawe ni aidha Mercedes-Benz S600, BMW 7 series, Audi A8 au A6, Mercedes-Benz ML, BMW X5 series, Audi Q7, Toyota Prado, Toyota Land Cruiser au Nissan Pathfinder.
Rais Zuma amewahi kuwaoa wanawake watano ambapo mwanamke mmoja kati yao, Nkosazana Dlamini-Zuma, alimpa talaka mwaka 1998 wakati mke wake mwingine toka Msumbiji, Kate Mantsho, alijiua mwenyewe mwaka 2000.
Hivi sasa Zuma anaishi na wake zake watatu Gertrude Sizakele, Nompumelelo Ntuli (MaNtuli) na Thobeka Stacie Madiba.
Zuma pia ana wachumba wawili ambao amepanga kuwaoa katika siku za karibuni
Pinda amsimamisha Magufuli ubomoaji wa majengo
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amemsimamisha Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli kusitisha kwa muda zoezi la bomoa bomoa za nyumba na majengo yaliyojengwa kwenye hifadhi ya barabara hadi hapo serikali itakapotoa tamko.
Agizo hilo alilitoa jana Wilayani Chato alipokuwa akizungumza na wananchi.
Pinda alimtaka waziri huyo kusitisha kwa muda zoezi hilo baada ya kutishwa na kasi yake utendaji wa waziri mwenye dhamana.
Alisema ni vyema zoezi hilo Waziri Magufuli akalisimamisha kwa muda, ili tathmini ifanywe nchi nzima kubaini majengo na nyumba zitakazobomolewa na kuepusha malalamiko kutoka kwa wananchi.
Hata hivyo Waziri Pinda alimsifu Waziri Magufuli kwa kufanya kazi nzuri na
kubwa na anaisimamia kikamilifu.
Waziri Pinda dametoa agizo hilo baada ya wananchi wengi kulalamikia zoezi hilo la ubomoaji wa nyumba.
Waziri Magufuli alitoa agizo kwa wale wote wenye majengo, mabango yaliyokuwa kwenye hifadhi ya barabara abomoe nyumba hizo ili kupisha upanuzi wa barabara.
Tayari nyumba kadhaa zimeshabomolewa kupisha upanuaji wa baraba hizo.
Simba azua varangati -Mbagala
WAKAZI wa maeneo ya Mbagala Kizuiani, Rangitatu na maeneo mengine ya karibu jana waliingia katika wasiwasi mwingine wa kuhofia kuondoa uhai wao baada ya Simba kuvamia maeneo hayo.
Wasiwasi mkubwa ulitanda kwa wakazi hao kuanzia majira ya asubuhi jana baada ya kuikia ngurumo ya Simba jike likilia kwa kutoa ngurumo la kuashiria alikwua maeneo hayo.
Wakazi hao walikumbwa na dhoruba hiyo na kufanya wakimbie huko na huko kunusuru maisha yao.
Ilifahamika kuwa kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Abdallah alimuona Simba huyo na kupishana naye majria ya alfajiri alipokuwa akienda kisimani kuchota maji huko maeneo ya mtaa wa Kimbangulile eneo mabalo liko karibu na mto Mzinga.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Bw. Kessy zilisema kuwa awali baadhi ya watu walimuona Simba huyo lakini hawakuweza kuthitisha kutokana na giza lililokwua limetanda lakini kadri kulivyozidi kupambazuka ngurumo zake zilizidi kusikika na wakazi wa maenejno hayo kubaini kuwa walikuwa na mnyama huyo katika mtaa huo.
Hivyo kutokana na hilo kijana mmoja aliyetambulika wka jina la Nassoro Allly alianza kumfurumusha Simba huyo kwenye gofu la nyumba dambalo lilikuwa halijamalizika kiujenzi ambako alikuwa amejificha na hatimaye alimruki maeneo ya shingoni na kujeruhiwa vibaya na simba huyo.
Alisema baada ya kuhakikisha ukweli huo alipiga simu polisi kwa msaada zaidi ambapo askari watano wa Kituo cha Polisi Kizuiani walifika hapo majira saa 1:30 na kuanza kumsaka kwenye maficho yake na kumpiga risasi bila mafanikio kutokana na bunduki aina ya SMG kuonekana kutomudu kumuua mpaka zilipotumika silaha kubwa zaidi
Alsiema samba huyo aliweza kuuwa majira ya Saa 2 asubuhi na wananchi wa maeneio hayo kupiga shangwe kwa kufanikiwa kuuawa kwa sima huyo.
Hata hivyo NIFAHAMSIHE iliabarishwa na mpasahji habari aliyekwua eneo la tukio kuwa kioja kilitokea wka wakazi hao kuonekana kuanza kufanya fujo kugombania viungo kwa matumizi yao wanayoyafahamu huku wengine wakidai kutaka kuchukua nyama na vurugu ikatanda maeneo hayo hadi askari polisi walipowatawanya wananchi hao kwa kurusha risasi hewani na kukimbia ambapo awali walilizingiri gari la polisi lililobeba mnyama huyo.
Hata hivyo baadhi ya wakazi waliokuwa wastaarabu waliendelea kufanya fujo hizo na hatimae walienda hadi kituo cha polisi cha Kizuiani kwa maandamdano na kuimba nyimbo 'tunamtaka simba wetu', wakijaribu huku wakijaribu kumchukua kwa nguvu simba huyo hivyo polisi walilazimika kumepelekea kusikojulikana
Wanawake wazichapa hadharani kugombania mteja
KATIKA hali isiyo ya kawaida wanawake wawili ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja wamejikuta wakizichapa hadharani kugombania wateja eneo la Kariakoo jijini.
Wanawake hao ambao wanaojishughulisha na kuuza uji, walishikana mikononi majira ya saa 3 leo kugombania wateja huku kila mmoja akidai ni wake.
Hata hivyo mteja waliyekuwa wakimgombania kutokana na utu wake alilazimika kununua uji huo vikombe viwili kwa kile alichodai kumridhisha kila mmoja kununua bidhaa yake hiyo.
Biashara hiyo ya uji imekuwa na chati hasa maeneo ya jiji ambapo wanawake wamekuwa wakipitisha uji wa aina mbalimbali ukiwemo wa ulezi, mchele na muhogo na wamekuwa wakitembeza mitaani majira ya asubuhi na jioni kujitafutia riziki.
Majeshi ya Gaddafi yazuia waasi
Libya
Majeshi ya serikali ya Libya yanasogea kuelekea kwenye bandari ya mafuta ya Ras Lanuf, yakiwasukuma waasi upande wa magharibi.
Mji wa Bin Jawad, uliopo kilomita 50 kutoka Ras Lanuf, sasa unadhibitiwa na majeshi yanayomtii kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.
Umoja wa Mataifa umemtaja aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Jordan kama mjumbe wake nchini Libya, ambapo waasi wanaompinga Gaddafi wakipambana katika wiki yao ya tatu.
Umoja huo pia ulisema, takriban watu 200,000 wamekimbia ghasia hizo.
Unatoa wito wa kutolewa dola za kimarekani milioni 162 ili kusaidia watu 600,000 wanaoishi ndani ya Libya watakaohitaji msaada wa kibinadamu, na pia watu 400,000 wanaoondoka nchini humo kwa muda
Hague aliidhinisha askari kwenda Libya
Watu wenye silaha Libya
Watu wenye silaha Libya
Vyanzo vya wizara ya mambo ya nje ya Uingereza vimeiambia BBC mpango uliovurugika wa vikosi maalum kutoka Uingereza SAS kwenda Libya uliidhinishwa binafsi na waziri wa mambo ya nje William Hague.
Askari hao sita waliachiwa huru pamoja na mtu mmoja aliyetambuliwa kama ofisa kutoka wizara ya mambo ya nje ya Uingereza siku mbili baada ya kutiwa mbaroni mashariki mwa Libya.
Waliondoka Malta kupitia manowari ya kivita ya HMS Cumberland Jumapili usiku.
Waziri wa mambo ya nje anatarajiwa kutoa taarifa kuhusu mpango huo siku ya Jumatatu mchana bungeni.
Askari hao walishushwa na helikopta mashariki mwa Libya lakini wakatekwa na wapiganaji wa upinzani na kukutwa wakiwa wamebeba silaha, risasi, ramani na hati za kusafiria kutoka nchi nne tofauti.
Katika taarifa yake ya awali Bw Hague alisema: " Askari hao walikwenda Libya kufanya mawasiliano na upinzani."
'Mawaziri waibiwa' Ivory Coast
Nyumba za mawaziri zapekuliwa
Vijana na mjeshi ya usalama nchini Ivory Coast yamepekura nyumba za "mawaziri" walioteuliwa na Alassane Ouattara, anayekubalika zaidi kuwa Rais.
Mashariki mwa nchi hiyo, waliokuwa waasi wanaomwuunga mkono Bw Ouattara dhidi ya mpinzani wake, Laurent Gbagbo, wameuteka mji wa Toulepleu.
Ivory Coast imekuwa katika ghasia tangu upigaji kura uliofanyika mwezi Novemba, Bw Gbagbo alipokataa kumkabidhi madaraka Bw Ouattara.
Ghasia hizo zimesababisha kutolewa kwa onyo la kuwepo mgogoro wa kibinadamu kutoka kwa mashirika ya kutoa misaada.
Walioshuhudia huko Abidjan walisema katika siku za hivi karibuni makundi ya vijana yamekuwa yakivamia nyumba za maafisa walio washirika wa Bw Ouattara na kuondoka na mali zao, huku polisi wenye sare zao wakiangalia tu.
Maafisa hao wamekuwa wakikaa na Bw Ouattara wakiwa chini ya Umoja wa Mataifa katika hoteli moja mjini humo.
Wote wawili Bw Ouattara na Bw Gbagbo wametaja majina ya baraza lao la mawaziri- waziri mkuu wa Bw Ouattara ni aliyekuwa kiongozi wa waasi Guillaume Soro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment