KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, February 19, 2011

Luteni Kanali Kibibi afikishwa mahakamaniWaathiriwa wa ubakaji nchini Congo
Mwendesha mashtaka mmoja nchini Congo, ametoa wito mahakama nchini humo kutoa adhabu ya kifo kwa wanajeshi watano ambao wanatuhumiwa kuhusika na visa vya ubakaji na uhalifu dhidi ya binadam.

Wanajeshi wengine watano huenda wakahumukiwa kifungo cha hadi miaka 20 gerezani.

Afisa huyo mwandamizi anayekabiliwa na mashtaka ni Luteni Kanali Daniel Kibibi, ambaye anatuhumiwa kuidhinisha wanajeshi wake kuwadhulumu kina mama na watoto mjini Fizi, Mashariki mwa Congo mwezi uliopita, kulipisa kisasi kuauwa kwa mmoja wao.

Kibibi amekanusha mashtaka hayo na kusema wao walikuwa wakijaribu kuthibiti machafuko yaliyokuwa yamedumu kwa zaidi ya saa 9 mjini Fizi.

Waendesha mashtaka wanasema karibu wanajeshi wote 150 waliokuwa chini ya Luteni Kanali Kibibi, walitekeleza uhalifu huo

No comments:

Post a Comment