KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, February 19, 2011

Kilo 100 za mchele kwa walioathirika


SERIKALI imewasaidia wahanga wa mabomu yaliyotokea katika kambi ya JWTZ Gongolamboto kwa kuwasaidia vyakula kwa kuwapatia kila kaya gunia la mchele la kilo 100 pamoja na kuwasaidia gharama za mazishi.
Serikali imeweza kuwapatia wahanga hao ambao wamepoteza nyumba zao ili chakula hicho kiweze kuwakimu .

Akizungumza na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Maafa, Didas Masaburu amesema kuwa mbali na msaada huo pia serikali imeweza kutimiza lengo la kuwazika wale wote waliopoteza maisha katika tukio hilo.

ALisema itagharamia gharama zote za mazishi kwa wale wote waliopoteza maisha katika tukio hilo, kusafirisha kwa wale ambao hawatazikwa jijini Dar es Salaam hadi pale familia watakapoteua kuzikwa miili hiyo.

Mbali na serikali pia watu mbalimbali wamekuwa wakijitokeza kutoa misaada mbalimbali kuwasaidia wahanga hao wa Gongolamboto

No comments:

Post a Comment