KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, February 19, 2011

Amuua Mama Yake Kwa Sababu ya PlaystationBaada ya mama yake kuificha Playstation yake, kijana mmoja wa nchini Marekani alimuua mama yake kwa kutumia nyundo na kisha alijaribu kuiteketeza maiti yake kwa kuibanika kwenye jiko la oveni.
Kendall Anderson mwenye umri wa miaka 16 wa Philadelphia, Marekani amekiri kumuua mama yake kwa kumtandika na nyundo mara 20 alipokuwa amelala kwasababu aliificha Playstation yake.

Kendall aliiburuza maiti ya mama yake hadi jikoni na kujaribu kuiteketeza kwa kuichoma moto kwenye jiko la oveni ili kuigeuza majivu.

Baada ya jitihada zake kushindikana, Kendall alitumia mguu wa kiti kuitandika maiti ya mama yake kichwani, aliiburuza hadi nje na kuifunika kwa takataka.

Katika ripoti ya polisi, Kendall akikiri kufanya mauaji hayo alisema kuwa siku ya tukio alijibishana na mama yake kwa zaidi ya lisaa limoja na nusu alipoificha Playstation yake.

Mama yake alipoenda kulala ndipo alipokamilisha mauaji yake kwa kumtandika na nyundo kichwani mara 20.

Kufuatia kukiri kwa Kendall kufanya mauji hayo, mahakama ya Philadelphia imeamuru Kendall afunguliwe mashtaka ya mauaji na mashtaka ya kuinyanyasa maiti.

Kendall akijitetea mahakamani alisema kuwa anajuta kumuua mama yake na kuongeza "Najuta kumuua mama yangu, nimemmiss sana alikuwa ni mtu pekee aliyekuwa akinijali".

No comments:

Post a Comment