KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, February 19, 2011

TSPCA yasaidia wanyama walioathirika Gongolamboto


CHAMA cha kusaidia haki za Wanyama nchini[TSPCA] kimefika eneo la wahanga na kuwasaidia wanyama walioathirika katika zoezi zima la mlipuko wa mabomu.


Waataalamu hao wameweza kusaidia wanyama 135 ambao wameonekana kuathirika kwa milipuko hiyo ambao wanyama hao wamegundulika kuathirika macho.

Pia wamegundua wengi wamepata tatizo la kiharusi, majeraha na homa kutokana na kadhia hiyo.

Wanyama hao wakiwemo ng’ombe, mbuzi, mbwa na wengineo waliweza kupatiwa chanjo mbalimbali.

“tumeona tujitokeze kusaidia wanyama kama watu wanavyojitokeza kusaidia binadamu na sisi tumeguswa na wanyama hawa walivyoathirika kwa kuwa wanyama nao wana haki ya kuishi kama wengine” walisema

No comments:

Post a Comment