KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Waziri wa Misri aishutumu Marekani

Waziri wa mambo ya nje wa Misri ametupilia mbali wito kutoka Marekani wa kutaka kuongeza kasi ya kufanya mabadiliko ya kisiasa.

Waandamanji Cairo


Akikataa madai ya Marekani kuondoa hali ya hatari, Ahmed Aboul Gheith amesema Marekani "isiweke" mamlaka yake katika "nchi kubwa".

Maelfu ya wananchi wa Misri wamekuwa wakiandamana tangu Januari 25, wakitaka rais Hosni Mubaraka kuondoka madarakani.



Maelfu ya wananchi wa Misri wamekuwa wakiandamana tangu Januari 25, wakitaka rais Hosni Mubaraka kuondoka madarakani.


Waziri Geith na waziri Clinton

Maandamano hayo siku ya Jumatano yamlifika hadi katika bunge la Misri, huku ghasia na maandamano zaidi yakiripotiwa katika miji mingine.

Mkusanyiko wenye mwelekeo kwa sasa upo katika eneo la wazi la Tahrir, katikati ya jiji la Cairo, ambapo ndio kitovu cha maandamano hayo yanayoingia





siku ya 17.




Waandamanaji Cairo


Picha za televisheni siku ya Alhamisi zimeonesha umati ukielekea katika eneo hilo. Idadi ya watu inatarajiwa kuwa kubwa siku ya Ijumaa, baada ya waandaaji kuitisha mkusanyiko mwingine mkubwa.

No comments:

Post a Comment