KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Mashambulio yazuka Sudan Kusini

Maafisa wanasema watu wasiopungua 16 wameuawa baada ya waasi kushambulia jeshi la Sudan Kusini, na kuteteresha makubaliano ya kusitisha mapigano.


Harakati wakati wa upigaji kura


Wapiganaji wanaomtii Goerge Athor wamelipua magari mawili ya kijeshi karibu na mji wa Fangak, katika jimbo la Jonglei, kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la kusini.

Saini

Bw Athor aliamua kubeba silaha mwaka jana, kwa madai kuwa kulikuwa na wizi katika uchaguzi wa jimbo, lakini alitia saini makubaliano ya kusitisha vita mwezi uliopita.

Mapigano haya yanakuja wakati Sudan Kusini inajiandaa kutengana na upande wa Kaskazini.

Waasi 12

Asilimia 99 ya watu wa kusini walipiga kura ya kutaka kujitenga, katika kura ya maoni ya mwezi uliopita, kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyotangazwa wiki hii.

Msemaji wa jeshi la upande wa kusini Philip Aguer amesema wanajeshi wanne na waasi 12 wameuawa, lakini anahofia watu zaidi wamekufa.

kuchochea

"Tunasubiri taarifa kamili za waliopoteza maisha," amesema.

Wakati Bw Athor akiamua kuchukua silala, upande wa kusini ulimtuhumu kwa kutumiwa na upande wa kaskazini ili kuchochea ghasia na kuharibu kura ya maoni, tuhuma ambazo maafisa wa upande wa kaskazini unazikana.

No comments:

Post a Comment