KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Redio ya UN yafungwa rasmi Ivory Coast

Serikali ya Ivory Coast ya kiongozi anayetetea kiti cha urais Laurent Gbagbo imepiga marufuku rasmi matangazo ya redio ya Umoja wa Mataifa.


Laurent Gbagbo


Bw Gbagbo amegoma kuondoka madarakani baada ya uchaguzi wa mwezi Nomvemba mwaka jana, ambao jeshi la kulinda usalama la Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast linasema Alassane Ouattara alishinda.

Inasikilizwa zaidi

Mwandishi wa BBC John James anasema masafa ya FM ya redio wa Umoja wa Mataifa tayari yamefungwa tangu kuanza kwa sakata hilo la kisiasa, ingawa umoja huo ulikuwa ukitumia masafa yasiyo rasmi.

Amesema redio hiyo ndiyo inasikilizwa zaidi nchini humo.


Ghasia baada ya matokeo nchini Ivory Coast


Upatikanaji wa redio na televisheni za kimataifa umekuwa mgumu tangu matokeo ya uchaguzi yenye utata yatolewe.

Ilitangazwa siku ya Jumatano jioni kuwa masafa ya redio ya Umoja wa Mataifa yamefungwa.


Mwandishi wetu mjini Abidjan anasema redio hiyo ilikuwa inasikika kupitia masafa ya 95.3 FM ambayo siyo rasmi hadi siku ya Alhamisi asubuhi.


Alassane Ouattara

Bw Gbagbo bado ana udhibiti wa kituo cha televisheni cha taifa (RTI) kisicho kurusha matangazo yake kupitia mitambo ya satellite.

Kituo kingine TV Cote d'Ivoire ambacho kimeanzishwa hivi karibuni na upande wa Bw Ouattara kinarusha matangazo yake mjini Abidjan.

Bw Ouattarra amesalia ndani ya hoteli mjini Abidjan, akilindwa na majeshi ya kulinda usalama ya Umoja wa Mataifa pamoja na waasi wa zamani ambao bado wanadhibiti maeneo ya kaskazini ya nchi

Wanajeshi wa UN wakilinda hoteli aliyomo Bw Ouattara


Uchaguzi wa mwezi Novemba ulikuwa na lengo la kuiunganisha nchi hiyo, ambayo ilikuwa imegawanyika pande mbili za kaskazini na kusini tangu kuanza kwa mzozo mwaka 2002.

Mwezi uliopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, liliidhinisha wanajeshi 2,000 zaidi kwenda Ivory Coast kuongeza nguvu kwa wanajeshi 9,800 waliopo huko.

No comments:

Post a Comment