KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 12, 2011

Wasafirishaji Madawa ya Kulevya Watano Wanyongwa Iran


Wanaume watano waliopatikana na hatia ya kukamatwa na madawa ya kulevya nchini Iran, wameuliwa kwa kunyongwa.
Wanaume hao ambao majina yao wala nchi wanazotoka hazikutajwa, walinyongwa jana kwenye jela ya Khoramabad katika mji wa Lorestan, magharibi mwa Iran.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran, Aftab, wanaume hao walikamatwa na madawa ya kulevya wakati wakijaribu kuyasafirisha na kuyasambaza madawa hayo ya kulevya.

Tangu kuanza kwa mwaka huu, ndani ya wiki mbili jumla ya watu 41 wamenyongwa nchini Iran.

Watu wanaopatikana na hatia ya makosa ya mauaji, kuzisaliti ndoa zao, ubakaji, ujambazi au kusafirisha madawa ya kulevya, huhukumiwa adhabu ya kifo

No comments:

Post a Comment