KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 12, 2011

Aomba wadau nifahamishe wamsaidie mawazo


Mwanamke Grace [33] amejikuta akikosa amani ndani ya ndoa yake kutokana na kukosa mtoto katika ndoa yake aliyofunga miaka mitatu iliyopita.
Grace ni mwajiriwa wa wizara ya maji amekuwa akiilalamikia ndoa yake kutokana na mume wake kumpa maneno machafu pindi anapoonekana ameingia ndani ya nyumba yake kwa mume wake alishindwa uvumilivu.

Alidai mume wake alikuwa akimpa maneno makali kwa kuwa alikuwa hashiki mimba kitendo ambacho mume wake alikuwa hakipendi na kumuhimiza kila kukicha anataka mtoto ndani ya nyumba yake hiyo.

Anadai hali hiyo imekuwa ikimfanye akose raha na mume wake kumuonyeshe dhahiri kuwa ana mwanamke wa nje bila kumficha na alijaribu kumkanya alikuwa akimfokea na kumpa maneno ambayo hayapendezi.

Alidai kuwa mume wake kwa kuwa amekuwa na shauku kubwa ya kupata mtoto siku za hivi karibuni alikuwa akimkuta mara kwa mara akiongea na wanawake na kwenye simu na alipokuwa akimuuliza kwa upendo hapati majibu mazuri.

Alidai alikuwa akijibiwa”mimi nataka mtoto na wewe huna uwezo wa huo, huyu mwanamke nimemuomba anizalie mtoto mmoja” kama umeona huwezi kuvumilia utaamua la kufanya

Na siku moja aliweza kumbainishia wazi kuwa, ana mwanamke ana mahusiano nae nje ya ndoa yake kwa kuwa alikuwa akihitaji mtoto na kumuahidi kumzalia mtoto huyo .

Hali hiyo anasema amekosa amani ndani ya ndoa yake, na mume wake huyo alikuwa akiamua kurudi nyumbani hapo ama kutorudi na amekuwa hajui la kufanya juu ya hilo na kuhofia kutoa ripoti hiyo ukweni kwani angekuwa anaidhalilisha ndoa yake.

Hivyo ameweza kuzungumza na nifahamishe ili aweze kuwekwa kwenye mtandao huu ili wasomaji waweze kumpa mawazo mawili matatu ili aweze kuyafanyia kazi

No comments:

Post a Comment