KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 12, 2011

Jogoo Mwenye Hasira Amuua Mmiliki Wake


Jogoo mwenye hasira amelipa kisasi kwa kumuua mmiliki wake aliyekuwa akimlazimisha aingie ulingoni kupigana na jogoo mwenzake katika kamari ya kupiganisha kuku nchini India.
Jogoo huyo kwa kutumia viwembe vilivyokuwa vimefungwa kwenye miguu yake wakati wa kupiganishwa na jogoo mwingine, alimrukia mmiliki wake na kulirarua koromeo lake na kupelekea kifo chake hapo hapo.

Taarifa zilisema kuwa jogoo huyo alimuua mmiliki wake aliyetambulika kwa jina la Singrai Soren ambaye alikuwa akimlazimisha jogoo huyo arudi tena ulingoni kupambana na jogoo mwingine baada ya kushinda pambano lake la kwanza.

Taarifa zaidi zilisema kuwa kwa kawaida jogoo hupumzishwa kwa zaidi ya lisaa limoja kabla ya kupambanishwa na jogoo mwingine.

Lakini Soren kwa tamaa ya kujiingizia pesa nyingi kila jogoo wake anaposhinda alimlazimisha jogoo huyo arudi tena ulingoni ndani ya dakika chache na ndipo jogoo huyo alipomaliza hasira zake kwa kulirarua koromeo lake.

Katika kamari hiyo ya kupiganisha kuku, mmiliki wa kuku anayeshinda hupewa zawadi ya pesa sawa na TSh. 60,000/= pamoja na kupewa kuku aliyeuliwa kwenye pambano hilo kama kitoweo.

Maafisa wa polisi katika kijiji cha Mohanpur, Bengal wameanza msako wa kumtafuta jogoo huyo aliyeshinda mapambano manne hadi sasa ili waweze kumvua viwembe alivyovalishwa kwenye pambano lake la kwanza kabla hajamrarua mtu mwingine

No comments:

Post a Comment