KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Wanasiasa wa mrengo wa shoto wataka maendeleo mbadala



Wanasisa wa mrengo wa shoto katika kongamano la kijamii duniani linalofanyika mjini Dakar, wamesema leo, kuwa mataifa yaliyoendelea yanapaswa kufanyakazi kwa pamoja , wakisisitiza haja ya kuwa na aina nyingine ya maendeleo. Rais wa zamani wa Brazil Luis Inacio Lula da Silva na kiongozi wa chama kisoshalist nchini Ufaransa Martine Aubry wamekutana pembezoni mwa kongamano hilo kujadili kikao kijacho cha kundi la mataifa ya G20 na ushirikiano miongoni mwa mataifa yaliyoendelea.

Lula amewaambia waandishi wa habari kabla ya mkutano wao kuwa katika kundi la mataifa ya G20 inaonekana kana kwamba hakuna matatizo, na hayazungumzii kuhusu ukosefu wa ajira.

Aubry amesema kuwa viongozi hao wawili wamezungumzia pia uhusiano baina ya mataifa ya Amerika ya kusini na Afrika.

Konganano la 11 la jukwaa la kijamii, ikiwa ni jukwaa mbadala wa jukwaa la kiuchumi duniani lilofanyika huko Davos Uswisi wiki iliyopita , huwaleta pamoja wanaharakati wanaopinga utandawazi na ubepari.

Fatma Aloo ni mmoja wa wanaharakati kutoka Tanzania na akizungumzia kuhusu kongamano hilo mjini Dakar alikuwa na haya ya kusema.

Kiasi cha watu 10,000 waliandamana jana katika mitaa ya mji mkuu Dakar wakiunga mkono maandamano ya umma yaliyosambaa katika nchi za kaskazini mwa bara la Afrika, ikiwa ni kuakisi mzozo uliotokana na ubepari, ikiwa ni mada kuu ya kongamano hilo.

No comments:

Post a Comment