KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Balozi wa Uholanzi mjini Tehran aitwa nyumbani



Uholanzi imemwita nyumbani balozi wake nchini Iran ikiwa ni malalamiko rasmi kuhusiana na kunyongwa kwa mwanamke raia wa Uholanzi mwenye asili ya Iran. Wizara ya mambo ya kigeni ya Uholanzi imesema leo kuwa serikali inapinga ukosefu wa heshima dhidi ya familia ya Sahra Bahrami, ambaye amenyongwa mwishoni mwa mwezi wa Januari kwa kuhusika na biashara ya madawa ya kulevywa. Maafisa hadi sasa wameshindwa kuutoa mwili wake kwa familia yake kwa ajili ya mazishi. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 45 amekataliwa kuwasiliana na ubalozi wa Uholanzi nchini Iran, ambao hautambui uraia wa nchi mbili.

No comments:

Post a Comment