KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Wamachinga wa kigeni kusakwa


WIZARA ya Viwanda na Biashara wameanza kazi rasmi ya operesheni ya kuwakamata Wamachinga wa kigeni katika jiji la Dar es Salaam.
Wizara hiyo inaanza kampeni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kusaka wageni hao wanaojishughulisha na biashara hizo kinyume na sheria.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juzi kuhusiana na utekelezaji wa wizara hiyo.

Amesema operesheni hiyo itaanzia katika maeneo ya Kariakoo kwa kuwa kuwa eneo hilo limeonekana kuwepo kwa wageni wengi wanaojishughulisha na biashara hizo ambao hawastahili kufanya.

Pia amefafanua kuwa mbali na eneo hilo operesheni hiyo itaendelea katika maeneo mengine ya nchini kote.

Alisema mbali na kuwakamata pia watawafungulia mashitaka kutokana na makosa watakayokutwa nayo mbali na hilo.

Alisema wafanyabiashara wengi wa kigeni wanaoingia nchini wamekuwa wakiingia nchini kwa vigezo na maelezo ya kuwekeza na baadae kubadilisha na kujishughulisha na shughuli za kimachinga.

Pia waziri huyo aliwataka wananchi kutoa taarifa rasmi pale wanapowaona raia wa kigeni wakifanya biashara ndogo ndogo ili waweze kuwafuatilia na kuwakamata.

No comments:

Post a Comment