KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Mzazi afarikia zahanati, azuiliwa kwenda Amana


MWANAMKE Sabela Mganga [31] ameaga dunia katika zahanati binafsi iitwayo COH iliyopo Ukonga Mazizini jijini Dar es salaam, kwa kuishiwa damu baada ya kujifungua watoto mapacha katika zahanati hiyo.


Mwanamke huyo mara baada ya kujifungua watoto hao hali yake ilikuwa imebadilika na kuishiwa damu na daktari kumuandikia mama huyo ahamie katika hospitali ya Wilaya ya Ilala ya Amana kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo mwanamke huyo aliweza kuzuiliwa na muuguzi mmoja wa zahanati hiyo kwa kuwa mwanamke huyo alikuwa hajamalizia deni lake alilokuwa akidaiwa zahanati hapo lililofikia shilingi laki moja hamsini na tano elfu na mia nane, l55,800 kwa huduma ya kujifungulia katika zahanati hiyo.

Mwanamke huyo alifika katika zahanati hiyo Februari 5 mwaka huu na kuendelea kukaa katika zahanati hiyo hadi Februari 7 na hatimaye aliweza kufariki dunia juzi kutokana na kukabiliwa na uhaba huo wa damu aliokuwa nao baada ya kufanikiwa kujifungua watoto wake mapacha

No comments:

Post a Comment