KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Viongozi wa zamani hawatakiwi Tunisia


Maandamano Tunis


Nchini Tunisia mamia ya waandamanaji, wamejiunga katika kupaza sauti bila kufanya ghasia zozote, katikati ya mji mkuu, Tunis, wakiwachagiza washirika wa Rais aliyeangushwa, Zine al-Abidine Ben Ali kutong'ang'ania madaraka.

Mazungumzo yanaendelea kati ya mawaziri walioteuliwa katika serikali mpya ya muda ya umoja wa kitaifa, ambao wamekataa kukubali wadhifa wao.

Majadadiliano hayo yamefuatia mgawanyiko kuhusiana na nafasi muhimu za uwaziri walizopewa wale waliokuwemo katika serikali ya zamani.

Mmoja wa mawaziri wapya, mpinzani wa zamani, Slim Amamou ameiambia BBC, serikali inahitaji watu wenye ujuzi kuandaa uchaguzi.

Naye katibu Mkuu wa Muungano wa nchi za Kiarabu, Amr Moussa, amewaonya viongozi wa nchi za Kiarabu, wanakabiliwa na ghasia kama zilizosababisha kuangushwa kwa utawala wa Rais Ben Ali wa Tunisia.

Akizungumza katika mkutano wa kiuchumi kwa nchi za Kiarabu nchini Misri, kwamba nchi za Kiarabu zinasumbuliwa na umasikini.

Kwa viongozi wa Kiarabu, mkutano huu wa kiuchumi ni nafasi nzuri ya kwanza kukutana na kuzungumzia matukio ya Tunisia, kama yanaweza kutokea katika nchi zao.

Katibu huyo Mkuu wa Muungano wa nchi za Kiarabu, amewaonya viongozi wa mataifa ya kiarabu kwamba, ukosefu wa ajira, umasikini na mdororo wa kiuchumi, unagubika maisha ya kila siku ya nchi za Kiarabu.

"Mapinduzi ya Tunisia hayako mbali nasi," aliuambia mkutano huo.

Na awali akitoa hutuba ya kufungua mkutano huo, Bw Moussa, alitaka mageuzi ya uchumi na kisiasa yaende sambamba.

Katika kile kinachoonekana hali bado si shwari nchini Tunisia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia, inaarifiwa alirejea nyumbani kutoka katika kikao hicho, kabla ya mkutano kamili haujaanza

No comments:

Post a Comment