KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

DUCE wafata nyayo


WANAFUNZI wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE), wameanza mgomo kwa kutoingia madarasani kwa madai ya kucheleweshewa fedha zao za kujikimu.


Wanafunzi wapatao zaidi ya 13oo walianzisha mgomo huo jana chuoni hapo majira ya asubuhi na kukusanyika kwa lengo la kuandamana.

Wanafunzi hao walidai kucheleweshewa fedha zao za kujikimu za awamu ya pili iliyoanza Januari 15, mwaka huu.

Hata hivyo Makamu Mkuu wa chuoni hap, Profesa Nyikomba Babu, aliwashauri wanafunzi hao kusitisha mgomo huo kwa kuwa alidai leo wataanza kulipa fedha hizo.

Pia alipokuwa akizungumza na nifahamishe mkuu huyo alikiri kucheleweshwa kwa fedha hizo kwa wanafunzi hao na kufafanua wanafunzi hao wanatakiwa wapewe kila mmoja Shilingi 300,000/= kwa ajili ya fedha za kujikimu.

Alisema tayari fedha hizo zimeshaingizwa katika akaunti ya chuo

No comments:

Post a Comment