KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Baba auwa watoto wake wanne, kisha ajiua


MKAZI wa kijiji cha Gekrumu Wilayani Karatu, mkoani
Arusha, amechukua uamuzi wa kuwauwa watoto wake wanne kisha na yeye mwenyewe kujiua kwa kile kilichodaiwa kutokana na wivu wa mapenzi.

MWanaume huyo alitambulika kwa jina la Evance Damiani (43) mkazi wa kijiji hicho aliamua kufanya hivyo baada ya kukosana na mkewe kutokana na sababu za kimapenzi.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea usiku wa kuamkia juzi nyumbani kwa Evance baada kuona mkewe amekimbia kusikojulikana alichukua shoka na kuanza kuwacharanga watoto wake kutokana na hasira alizokuwa nazo baada ya mkewe huyo kukimbia kusikojulikana.

Mara baada ya kuwaua watoto hao, nae alichukua uamuzi wa kujiuua.

Hata hivyo taarifa iliyotolewa na polisi ilisema maiti zote tano zilikutwa asubuhi iliyofuata nyumbani kwake na kuzikusanya kwa uchunguzi na kuendelea kumsaka mwanamke huyo.

Aidha imedaiwa kuwa marehemu Evance alikuwa na mzozo wa muda mrefu na mkewe huyo kwa kuhisi kusalitiwa na mkewe na hivyo kutokea kwa mizozo ambayo mara kwa mara ilikuwa ikitokea kati yake na mkewe.

Watoto walioweza kupoteza maisha ni Theophil Damian (11), Ritha Damiani (9) na wengine walikuwa mapacha walitambulika kama Jigimu Damiani na Theodore Damiani wana umri wa miaka 6

No comments:

Post a Comment