KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Uwanja wa ndege mjini Moscow walipuliwa

Uwanja wa ndege wa Domodedovo wa Moscow umetikisika baada ya kutokea mlipuko wa bomu ambapo msemaji wa uwanja huo alisema watu 35 wamefariki dunia.

Zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa- 20 wakiwa katika hali mbaya sana kutokana na mlipuko huo, ambapo ripoti zinasema shambulio hilo limefanywa na mtu aliyejitoa mhanga.

Mchunguzi mkuu wa Urusi alisema magaidi ndio wamehusika na shambulio hilo.

Uwanja huo, ambao una shughuli nyingi katika mji mkuu wa Urusi, upo kilomita 40 kusini-mashariki mwa mji huo

Mwathirika wa mlipuko wa bomu, Moscow


Rais Dmitry Medvedev alisema waliohusika na shambulio hilo watasakwa mpaka wapatikane.

Ameamuru kuwepo na usalama zaidi kwenye mji mkuu, kwenye viwanja vya ndege na vituo vengine vya usafiri, na pia ameitisha mkutano wa dharura na maafisa waandamizi.

Pia imebidi kuahirisha safari yake ya kuhudhuria mkutano wa uchumi duniani huko Davos.

Mwandishi wa usalama wa BBC Gordon Corera alisema mashaka moja kwa moja yataelekezwa kwa wapiganaji kutoka mji wa Caucasus.

Corera alisema, wapiganaji wanaopambana Caucasus wanajua namna mwonekano wa Rais na waziri mkuu wa kuwa na jamii salama ilivyo muhimu kwao, na hivyo kuutikisa usalama huo ni lengo lao kuu.

Mwezi Machi mwaka jana mfumo wa treni za chini ya ardhi kwenye mji mkuu wa Urusi ulitikiswa na wanawake wawili waliojitoa mhanga kutoka mji wa Dagestan, na kusababisha vifo vya watu 40 na kujeruhi zaidi ya 80.

No comments:

Post a Comment