KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 12, 2011

Palestina yajibu kuhusu 'nyaraka za siri'

Wakimbizi wa Kipalestina, Lebanon
Maafisa wa Palestina wameishutumu al-Jazeera kwa kupotosha, baada ya kutoa taarifa za siri zilizokusudia kuonyesha nchi hiyo kuwa na maridhiano makubwa na Israel.

Rais Mahmoud Abbas alisema siri hizo zimechanganya kwa makusudi misimamo ya Palestina na Israel.


Nyaraka hizo zinasema kuwa Palestina iliikubalia Israel kubaki na eneo kubwa la mashariki mwa Israel wanalomiliki kinyume cha sheria- jambo ambalo Israel imelikataa.

BBC imeshindwa kuthibitisha binafsi nyaraka hizo.

Al-Jazeera ilisema ina rekodi 16,076 za siri za mikutano, barua pepe, na mawasiliano baina ya Palestina, Israeli na viongozi wa Marekani, baina ya mwaka 2000-2010.

Inaripotiwa Wapalestina wamependekeza kuundwa kwa kamati ya kimataifa ili kuhodhi maeneo matakatifu ya Kiislamu Jerusalem, na kupunguza idadi ya wakimbizi wanaotaka kurejea kufikia 100,000 kwa kipindi cha miaka 10.

Nyaraka hizo zinaaminiwa kutolewa kwa upande wa Palestina.

Bw Abbas, anayetarajiwa kufanya mazungumzo ya amani ya Mashariki ya kati siku ya Jumatatu na Rais wa Misri Hosni Mubarak, alisema mazungumzo ya amani yamefanyika kwa uwazi, na viongozi wenzake wa kiarabu walikuwa wakijua kila kilichoendelea.Gaza

Akinukuliwa na shirika la habari la Reuters, alisema akiwa Cairo, " Kinachokusudiwa ni kutuchanganya. Nilishuhudia jana wakiwasilisha taarifa kama Palestina lakini walikuwa Israel...kwa maana hiyo hilo limefanywa kusudi."

Wakati huo huo, msemaji wa serikali ya Palestina, Yasser Abed Rabbo, alikataa kusema iwapo nyaraka hizo ni za kweli au la.

Alisema " Leo al-Jazeera imechapisha kwa kile kinachoita nyaraka zilizotolewa na wakurugenzi wa mapatano wa PLO."

" Hatutajadili uhalali au kutokuwa na uhalali wa nyaraka hizo."

Mhariri wa BBC wa Mashariki ya Kati Jeremy Bowen alisema kauli ya Palestina inaashiria mtikisiko mkubwa ambao nyaraka hizo za siri zinaweza kusababisha kwa Bw Abbas na wenzake.

Serikali ya Palestina kwa sasa itabidi kuwashawishi raia wa Palestina kwamba uamuzi huo ulifanyika kwa faida yao, hasa ambapo wengine wataona nyaraka hizo kama namna nyingine ya kuwadhalilisha.

Msemaji wa kundi la Hamas, ambalo linadhibiti ukanda wa Gaza na ni mpinzani wa chama cha Fatah cha Bw Abbas, alisema nyaraka hizo zilidhihirisha "ubaya wa serikali ya Palestina, na kiwango cha ushirikiano wao na umiliki wa Israel."

No comments:

Post a Comment