KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Upinzani Tunisia waikaribisha hotuba ya rais Ben Ali

Rais Zine El Abidine Ben Ali asema ataondoka madarakani 2014




Watunisia wameanza siku ya leo wakiwa katika nchi inayoonekana kuwa tofauti kabisa baada ya rais wa nchi hiyo kutangaza kipindi maalum ambapo ataondoka madarakani.

Zine al-Abidine Ben Ali, ambaye ameiongoza Tunisia kwa zaidi ya miaka 23, amesalimu amri kutokana na mbinyo wa ghasia za wiki kadha na kutangaza katika hotuba aliyoitoa kwa njia ya televisheni kuwa ataondoka madarakani mwaka 2014, ameamuru polisi kuacha kuwashambulia waandamanaji na kuahidi uhuru wa vyombo vya habari.

Watunisia ambao wameishi katika hali ya kuwekewa mipaka ya uhuru wao na utawala wa rais Ben Ali, walipepea bendera, walicheza, walipiga honi za magari na kuimba wimbo wa taifa

Hisia za wananchi

Hatukutarajia hili katika hotuba yake, amesema Mohammed Ali, anayetoka katika eneo la Lafayette katika mji mkuu Tunis ambako saa chache kabla polisi walimpiga risasi mtu mmoja wakati wa maandamano. Kitu muhimu ni uhuru, uhuru, uhuru.

Sonia Ayari mtu mwingine ambaye alikuwa akisherehekea mitaani, amesema: Tunaupongeza ujasiri wa Ben Ali, hata kama umechelewa.

Katika kitongoji cha Al Omran nje kidogo ya mji mkuu Tunis , wanawake wameingia mitaani , wakipuuzia amri ya kutotoka nje iliyowekwa siku moja kabla, na kuimba, Viva Ben Ali.

Hata katika miji kadha ya Tunisia ambako watu kadha wameuwawa katika mapambano na polisi , watu wengi, japo si wote, walikuwa na furaha.

Katika mji wa Sidi Bouzid , mji ambako wimbi la ghasia lilianzia wakati mtu mmoja ambaye hana kazi alijichoma moto mwezi Desemba mwaka jana katika hatua ya kuonesha upinzani wake, watu wachache waliimba na kucheza kwa furaha, kwa mujibu wa wanaharakati wa vyama vya wafanyakazi.

Televisheni ya taifa , ambayo kwa kawaida haithubutu kuikosoa serikali, ghafla ilibadilika . Watu kama mpinzani mkubwa wa Ben Ali, Taoufik Ayachi pamoja na kiongozi wa chama cha waandishi habari ambaye aliondolewa madarakani Naji Baghouri , ambao hapo zamani walikuwa hawawezi kuonekana katika televisheni hiyo, walionekana jana jioni. Watazamaji waliweza kwa mara ya kwanza kuona mjadala wa wazi kuhusu vyombo vya habari nchini Tunisia ambapo mtu mmoja ameweza kumkosoa wazi mmoja wa jamaa ya familia ya rais.



Machafuko Tunisia

Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Ghasia zimekuwa zikiendelea Tunisia kwa wiki kadhaa Baada ya karibu mwezi mzima wa machafuko ambayo kimsingi yalilenga kuhusu ukosefu wa ajira, rais wa nchi hiyo alijitokeaza katika televisheni katika hatua ya kupunguza hali ya wasi wasi.

Katika hotuba yake kwa taifa Ben Ali ameahidi kutowania kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa mwaka 2014 na kusema majeshi hayapaswi tena kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji.

Kufuatia ukosoaji mkubwa kutoka mataifa ya nje kuhusu demokrasia nchini humo, Ben Ali ameahidi kuanzisha uhuru kamili wa habari na upatikanaji wa mtandao wa internet na kuahidi mageuzi kadha. Mbunge Ahmed Ben Brahim, kiongozi wa chama cha zamani cha kikomunist Ettajdid amesema , hotuba hiyo ni muhimu na inatoa majibu ya maswali yaliyozushwa na chama chake.

Hotuba hii inatoa nafasi ya uwezekano, amesema Mustapha Ben Jaafar, mkuu wa chama cha jukwaa la kidemokrasia na uhuru

No comments:

Post a Comment