KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Serikali yatakiwa kufafanua kupanda kwa umeme


ASKOFU Mkuu wa Umoja wa Makanisa ya Pentekoste Tanzania (FPCT), David Batez, ameitaka serikali kufafanua sababu za upandishaji wa gharama za umeme, ambao umekuwa mwiba kwa Watanzania wengi wenye kipato cha chini kushindwa kumudu gharama za maisha.

Kauli hiyo aliitoa kufuatia, Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji (Ewura) kukubali kupandisha bei umeme kwa asilimia 18.5 kwa madai kuwa ongezeko la gharama ya mafuta imepanda.

Akifafanua hoja yake Askofu Batez alisema serikali kama ina nia na wananchi wake kuwapatia maisha bora, lazima ifafanue kwa kina sababu za msingi za kupandisha bei ya umeme.
Alisema sababu za awali haziwaridhishi wananchi.

Batez alisema ni vema serikali ikatafuta njia mbadala ya kushusha gharama hizo, kwa kubuni mbinu za utumiaji wa nishati.
“ Sasa hivi wananchi hawajaridhika na sababu za kupanda umeme na ndiyo maana wanalalamika, ukiona hivyo ujue hawaridhiki na kupaa kwa gharama hizo,” alisema Batez.

Bateza alisema kama gharama za umeme wa mafuta nin kubwa basi serikali haina budi kujikita zaidi kwa matumizi ya gesi asilia.

“Serikali inaweza kuwahamasisha wananchi waweze kutumia gesi ya songosongo na makaa yam awe iliu wapunguze gharama” alisema.

“Kila mwaka serikali inapandisha gharama za umeme, halafu inasema itahakikisha Watanzania wanaishi maisha bora, wakati hali hiyo inachangia umasikini,”alisema.

Wakati huo huo, Askofu Batez alilaani na kupinga vikali kitendo kilichofanywa na jeshi la polisi mkoani Arusha kwa kujichukulia sheria mkononi na kumwaga damu zisizo na hatia.

Alisema, kama wafuasi wa Chademaau chama kingine chochote wameamua kuandamana kwa lengo la kutoa hisia zao, hakuna sababu ya kuwaingilia na kuwafanyia fujo

No comments:

Post a Comment