KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 12, 2011

Shein kuongoza Mapinduzi leo


RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, leo anaongoza maadhimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar visiwani humo.
Sherehe hizo zinaadhimishwa katika Uwanja wa Aman uliopo mjini Zanzibar ambapo Shein ataongoza maelfu wa Wazanzibar katika sherehe hizo.

Sherehe hizo za leo ni za historia ambapo ni kwa mara ya kwanza sherehe hizo zinaadhimishwa katika serikali ya umoja wa kitaifa.

Katika sherehe hizo Viongozi mbalimbali wa kitaifa wanatarajiwa kuhudhuria akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu, Federick Sumaye, na viongozi wengine wengi wakuu wastaafu watahudhuria sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment