KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Marufuku Mwanaume Kumshika Mkono Mwanamke


Wanamgambo wa kundi la Al-Shabbab wa nchini Somalia wametangaza kupiga marufuku wanaume kusalimiana kwa kushikana mikono, kutembea au kuongea na wanawake ambao hawana uhusiano nao.
Wanamgambo wa Al-Shabbab wametangaza kuwa ni marufuku mwanaume na mwanamke ambao hawana uhusiano wa kidugu kusalimiana kwa kushikana mikono, kuongea pamoja au kutembea barabarani pamoja.

Watu watakaokiuka sheria hiyo mpya watacharazwa bakora mbele ya hadhara au kutupwa jela au hata kuhukumiwa adhabu ya kifo.

"Hii sheria sio nzuri, najihisi kama niko chini ya ulinzi, nimeanza kuzipuuza salamu za wanawake ninaowajua kwa kuhofia adhabu ninayoweza kupewa", alisema Hussein Ali, mkazi wa mji wa Jowhar uliopo kusini mwa Somalia.

Hivi karibuni Al -Shabbab walipiga marufuku wanawake kutembea peke yao barabarani bila ya waume zao au ndugu zao wa kiume.

Wanamgambo wenye silaha wamekuwa wakiyasachi mabasi ili kuwatafuta wanawake wanaosafiri peke yao au wale waliovaa nguo zilizo nje ya maadili.

Chini ya sheria zilizotangazwa na Al-Shabbab wanawake wanatakiwa kuvaa nguo ndefu zinazoifunika miili yao au la wataambulia bakora mbele ya umati wa watu.

No comments:

Post a Comment