KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Jambazi lauawa, alivamia gesti kutaka kupora wapangaji


JAMBAZI moja kati ya wanne waliofika katika nyumba ya kulala wageni iliyotambulika kwa jina la Inn’s lodge, iliyopo Kigogo limeuawa na wenzake kujeruhiwa wakati alipovamia nyumba hiyo kwa minajiri ya kuwaibia wapangaji waliokuwa katika nyumba hiyo
Akizungumza na waandishi wa habari, wakati akitoa taarifa hiyo , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Bw. Charles Kenyela alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika nyumba hiyo.

Alisema jambazi hilo ambalo jina lake halijafahamika lilifka katika nymba hiyo kwa kujifanya mpangaji kwa takribani siku mbili mfululizo akiwa anajifungia katika chumba chake hicho alichopanga katika nyumba hiyo bila kuonekana akitoka nje.

Alisema juzi usiku wa saa 8 alionekana na wahudumu na kuwataka wahudumu wamfungulie mlango wan je kwa kuwa kuna wageni wake walikfika hapo kusasalimia na wahudumu hao hawakuafiki.

Kamanda Kenyela alisema, jambazi hilo alianzza majibishano na wahudumu hao akilazimisha kufunguliwa mlango huo na ghafla waliingia watu watatu wakiwa na silaha.

Alisema, watu hao walianza kupita chumba kimoja baada ya kingine mwa nyumba hiyo na kufanikiwa kuwapora wapangaji na makelele halianza kupigwa na wapangaji hao kuomba msaada wa raia wema.

Ndipo wananchi walipofika eneo hilo huku mmoja wa wananchi waliofika hapo alikuwa na bastola yake na kumfyatulia risasi jambazi hilo na aliweza kupoteza maisha papohapo na wengine walijeruhiwa vibaya na hali zao inadaiwa kuwa ni mbaya

No comments:

Post a Comment