KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, January 12, 2011
Papa Yohane Paulo II kuwa Mwenye Heri
Hayati Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili anatarajiwa kutangazwa Mwenye Heri, baada ya jopo la makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican, kuthibitisha kuwa alitenda muujiza, hatua ya mwisho inayohitajika katika kumfanya kuwa Mwenye Heri.
Baba Mtakatifu Benedikto wa Kumi na Sita ametangaza kuwa Papa Yohane Paulo wa Pili alimtibu mtawa wa Kifaransa ambaye alikuwa anaugua ugonjwa wa Parkinson. Papa Benedikto amekiita kitendo hicho kuwa ni cha kimiujiza.
Sherehe hizo zitakazofanyika Mei Mosi mwaka huu, zinatarajiwa kuwakusanya maelfu ya mahujaji huko Roma kumsheherekea Papa huyo, mzaliwa wa Poland, mmoja kati ya Baba Watakatifu maarufu zaidi.
Hatua ya kutangazwa Mwenye Heri ni ya mwisho kabla ya kutangazwa Mtakatifu, ambapo muujiza wa pili unahitajika. Papa Yohane Paulo wa Pili alianza kuwekwa katika mchakato wa kuelekea kuwa Mtakatifu, wiki chache tu baada ya kufariki mwaka 2005
KATI YA MALKIA ELIZABETH NA PAPA YOHANE PAULO 1
NARUDIA baadhi ya hoja tulizotoa, ingawa kichwa cha habari ni kipya(tutajadili mbele). Yako maswali mengi ambayo wasomaji wanauliza. Wapo mwanaotaka kujiunga na Freemasons, lakini nitawaeleza labda wakaulize wahusika kuhusu ‘taratibu’ za kujiunga. Pia najaribu kurudia baadhi ya viungo ili kuwaelewesha wasomaji wapya ambao wanahitaji kufahamu tulipoanza tulianzaje na tukafika wapi.
Kimsingi tulianza na makala ya kwanza kwa udadisi kuhusu tukio la septemba 11, 2001. Makala ile iliuliza swali kwamba Osama bin laden ni adui wa Marekani?(lakini jawabu likawa limebaki na swali, kama tuamini au tusiamini). Kisha tukafuta mfululizo wa makala za Osama bin laden ni gaidi? Tukaongelea kuhusu je ugaidi ni biashara huria?
Baada ya hapo ndipo tukajikita kuhusu siasa za Afghanistan kwa lengo la kutanguliza tunachojadili kuhusu Freemasons. Tulijadili namna Marekani na wshirika wake wanavyoitumia nchi hiyo kwa maslahi yao. Ndipo tukafika kwa hawa walokole wanavyoiangamiza dunia, iliulizwa ni walokole gani?
Jawabu ni kwamba siyo walokole tunaona huko mitaani bali ni wale wanaoundwa na taifa la Marekani. Tukajadili kuwa hilo ni tawi la Freemasons kwa maana ya moja ya uharibifu unaofanywa na waumini hao. Uharibifu ambao unatokea sasa kwa kisngizio cha ugaidi ni mkubwa sana. Inatosha tu kusema, tutaendeleza mada hizi kwa kungalia mengi kuhusu Freemasons.
Wiki jana kumekuwa na wsaomaji wapya na wale wanaofauatilia mfululizo huu. Wapo walioahidi kuendelea kusoma makala katika gazeti hili, nami nawakaribisha, nawaambia kusoma tu hakutoshi tunahitajika kupembua mambo kwa uyakinifu kabisa.
Pamoja na hayo, msomaji mmoja ameuliza swali kwamba ni nani mkuu wa Freemasons duniani? Kwa kuwa tulianza kudodosa mambo haya kitambo, basi jibu langu litakuwa katikati ya maelezo-kwani tusitake kumeza kama kinda la ndege. Tukumbushane kuhusu hili, kabla hatujaingia kwa Malkia Elizabeth.
Sote tunamfahamu Albino Luciani, ambaye alichaguliwa kuwa Papa wa kanisa katoliki.
Alichagua kuitwa jina la Papa Yohane Paulo I. Pamoja na kuchaguliwa huko, alijkuta akiongoza kanisa katoliki kwa siku 33 tu. Ni siku ambazo zilikuwa na mtafaruku ambao unaendelea hadi leo. Ni siku ambazo binadamu huyu angelikuwa hai,labda tungejua zaidi ya haya.
Ni siku ambazo tungelijua zaidi kuwa Freemasons hawawezi kuishi kwa kuwauzia waumini wake vinywaji na kukamilisha kuwa hiyo ndiyo ibada yao. Albino Luciani, mzaliwa wa Italia na binadamu aliyekuzwa katika imani ya kikristo ya kanisa katoliki. Ni binadamu ambaye leo tunatamani angekuwa hai ili atuambie nini kilitokea katika siku zake 33 za kuliongoza kanisa katoliki?
Kama siyo huyo, basi Roberto Calvi angelitueleza nini kilichotokea katika familia ya Freemasons, Mafia na Opus Dei katika siku 33 za utawala wa Papa Yohane Paulo I? kama ni vinginevyo basi tunahitajika kujua zaidi ya tunachokijua sasa. Tunatakiwa kujua, ingawaje kujua huko tu hakutoshi. Lakini pamoja na uhaba za mambo yenyewe kwakuwa yamekaliwa na baadhi ya watu, kwa hakika tutajua mengi tu.
David Yallop katika kitabu chake cha In God’s Name, alisema ‘ukitaka kuiba kwa ufasaha basi anzisha benki. Anataja kuwa benki ni ndiyo wizi mkubwa akuliko wote duniani, na ambao uliweza kugharimu maisha ya Papa Yohane Paulo I’. kwa mantiki hiyo nakwambia msomaji mpendwa, kanisa katoliki limeanzisha benki nchini. Je unaelewa ninachomaanisha?
Matafaruku ule ulipotokea hata Papa Yohane Paulo I uzalendo ukamshinda na kuahidi kuwalipua na kashfa zao ndipo yalimkuta mauti. Kwahiyo basi utendaji wa Freemasons unaendana na uanzishwaji wa Benki. Kuna Barclays,na Bank of England (ambayo iko tangu mwanzo wa mfalme wa Alexander The Great wa Uingereza.
Katika kitabu cha ‘History Of The Catholic Church; From Renaissance To The French Revolution’ cha Rev. James MacCaffrey, anaeleza sana kuhusu Albert Pike ambaye ndiye alikuwa mwalimu mkuu wa mafunzo ya kishetani na upagani wa Freemasons. Alikuwa kifundisha maudhui ya kfreemasonsa ambayo iliwachukua miongo kadhaa baadhi ya wanazuoni kubaini.
Alichofundisha ndiyo ujuio wa akina Adolf Hitler, Mapinduzi ya Ufaransa, kuibuka kwa USSR, kuongoza mafunzo ya Kirumi n. tukubaliane kuwa katika mafunzo mengi ya dini za kigeni hizi yanaambatana na eneo husika, kwa mfano Biblia imebandikwa historia nyingi za kirumi, Wayahudi (uzayuni wao na kabballah, ambako ndiyo mwanzo wa Freemasons tangu Waebrania.
Anson Phelps Stokes anaeleza namna freemasons walivyoanza shughuli huko Amerika, katika ukurasa wa 245 ‘The First regular Lodge of American Freemasons is believed to have been establish in Philadephia about 1720’. Ingawaje Ametumia neon ‘believed’ kwamba inaaminika, lakini jawabu sahihi ni kweli na ndivyo ilivyokuwa hata sasa.
Na tawala zote za Marekani tangu mwaka 1776 ni za Freemasons tangu kuanzishwa kwa taifa hilo na Rais George Washington. Rais huyu alikuwa mfuasi wa Freemasons, na maarufu kwa jina la ‘Worshipful Master’. Katika mafundisho yake mwalimu wa Freemasons Albert Pike ambayo anayaandika katika kitabu cha ‘Morals and Dogma’.
Tujadili hili; katika kichwa cha habari hapo juu nimeandika ‘kati ya Malkia
Elizabeth na Papa Yohane Paulo I’. nimefanya hivyo kwa dhumuni moja tu kwamba kuna tofauti kati ya hawa wawili ingawe wote ni waumini wa dini inayomuenzi kristo. Na ili kulazimisha hoja zake Albert Pike anataja kuna ‘master of Freemasons’ akimaaminsha Yesu Kristo.
Haishangazi kwani tunaelewa dhumuni ni kuwateka zaidi watu kama wanavyofanya kila kukicha. Huko nyuma niliuza hapa kwamba unajua kwanini unasijili simu yako? Ukijipa jawabu, nitakukumbusha kama nilivyodokeza wiki jana kuhusu ‘microchip’ ambao Rockefeller anataka tuwekewe bindamu wote ili wapate taarifa za kila mmoja.
Ukirejea suala la Papa Yohane Paulo I, inaelezwa alikusudia kulipua kashfa iliyolikabili kanisa katoloki hususan baada ya Freemasons kujipenyeza Vatican. Inaelezwa uzao huu wa kishetani ulijikia huko Isarel mwaka 1826 kwa kutoa namba zao za mawsiliano na zile zinazoheshimiwa(tutajadili safari nyingine).
Mnamo April 3, 2005 Sir Jayantilal Kashavji au Andy Chande, alijigamba kwamba katika uongozi wake wa miaka 50 ya Freemasons alitunukiwa tuzo na Malkia Elizabeth. Baada ya kuulizwa kwanini, akaeleza kuwa ni kutoka na uongozi mzuri na Malkia huyo alithamini uongozi wake.
Mangapi yametokea nchini Tanzania chini Freemasons? Ni kweli Al Qaeda walishambulia balozi za Marekani za Nairobi na Dar es salaam? Kuna ushahidi wowote ambao magaidi waliingia nchini na nyenzo na kufanya shambulizi. Wakubwa wetu hawa wanaficha nini hasa ambacho wenye nchi hatutakiwi kukijua?
Kwa mantiki hiyo basi Freemasons wamefanikiwa kututeka nyara kiakili kwa muda mrefu, na kwa kiasi kikubwa hatukujua kiwango cha mambo wanayoyatenda ndani mwetu…..lakini sasa tunajua, ingawaje hata kujua huko tu hakutoshi. Licha ya kwamba tumezungukwa na habari nyingi ambazo hazitupatii hekima. Na wametuteka wkani wamewashikilia watawala wetu!
Wakati Fulani William Shao alipata kuhoji tofauti ya ‘Sayansi na Unajimu’ (msome hapa; www.willyshao.blogspot.com). Kwa kifupi alihoji tofauti ya haya mambo. Katika kuhoji kwake wasomaji baadhi walidhani analeta mchezo, lakini ukiwauliza mbona mlitiwa hofu kwa ugonjwa KIMETA?
Hoja ya ‘Sayansi na Unajimu” ni pan asana, inakuta hata Nostradamus ambaye tunasadikishwa eti alitabiri mambo mengi yanayotokea sasa. Kwa taarifa yako huyo ni uzao wa Freemasons ambao walipanga kila jambo kwa muda wake kwahiyo alichotakiwa kukifanya ni kuleta kwa binadamu. Kimeta ni moja ya silaha ya kibaolojia na hatari iliyopata kutengenezwa na Freemasons.
Katika kurudia baadhi ya hoja ili kuwatendea haki wasomaji wapya, ni vema tukakumbusha kuhusu hili. Mahekalu na masinagogi yaliyoko Israel yanawahusisha Freemasons kwahiyo wanahistoria ndefu. Kuna msomaji aitwaye Jim wa Mbinga, alituma sms akitaja namba 666, kujadili hoja za kitabu cha ufunuo. Na akajaribu kuainisha 1 Mambo ya Nyakati 20: 6, Danieli 3:1-23 na ufunuo 13:16-18. Ni hoja nzuri.
Inazungumziwa sana mwenye ‘chapa’ katika aya hizo za ufunuo. Na ukipita barabar ya Morogoro (Morogoro Road) jirani na jengo la umoja wa vijana, utakuta msikiti wenye alama ya jeshi la Nazi. Ni alama ya waumini wa ibada za kishetani Freemasons (alama ya mawasiliano), lakini swali la kujiuliza hapa je wahusika wanajihusha na Freemasons? Tuliache hilo!
Soma hii; "Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na ahesabu ya mnyama huyo, maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita sitini na sita(666)”. Ufunuo wa Yohana 13: 18. Nasadiki(narudia) kwa dhati kuwa wale waumini wa dini hii wataweza kutupatia tafsiri kamili juu ya mambo hayo, Tunaambiwa 666 ni hesabu ya kibinadamu zaidi na mwenye akili na aihesabu hiyo kama ilivyo.
Namba 666 inahusishwa na ishara za siri za aliyekuwa mfalme wa Rumi Nero Caludius Caesar Augustus Germanicus( 37-68). Namba 666 inayohusishwa na utumwa wa mwanadamu na 666 imeelezwa katika kitabu cha 11 na cha 66 cha Biblia. Tukumbuke kitabu cha 11 ni Wafalme na cha 66 ni Ufunuo.
Na kitabu cha 11 cha Biblia ni 1 wafalme 10: 14. Ambacho katika matumizi ya namba 666 kinasema hivi "Basi uzani wa dhahabu iliyomfikia Suleimani mwaka mmoja ndio talanta mia sita sitini na sita (666). Tusome pia katika kitabu cha Mambo ya nyakati 9:13, Ufunuo 13:48. Katika kitabu cha Ezra 2;13 kunatamkwa namba 666.
Biblia inavitabu 66 Unaweza kuhesabu toka kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo. Je maana nyingine ufunuo ni mwisho. Kwa maana hiyo ibada za kishetani za kizazi cha Freemasons zinatufikisha mwisho? Kwanini freemasons waabudu huku wakiwatenga wanawake? Kwa maana nyingine tunaweza kujiuliza pia nafsi za Yakobo zilikuwa 666? (Mwanzo 46:26)
Narudia hizi pia; Kwanini mwanamke wa kiisrael alipangiwa siku 66? ( Mambo ya Walawi 12:5). Je hizo ni imani za Freemasons ambazo tunaambiwa zilijikita pia katika tamaduni za Waebrania kama tulivyoeleza awali? Na labda haya ndiyo aliyokuwa akiyakataa Papa Yohane Paulo I, na yanakubalika kwa Malkia Elizabeth alirithi kwa baba yake.
Na hili pia; Ukiitzama sarafu ya EURO inazo nyota 6 kamili, na fito 6 zimeshika nyota hiyo. Na Julai 20, mwaka 1999 bunge la kwanza lilifanyika barani humo na kupitisha maazimio kadhaa. Moja ya maazimio hayo ni kuchaguliwa kwa mwanamke aliyepanda mnyama kama alama yao ( Ufunuo 17:30). Simulizi zake zinaeleza sanamu la mwanamke lililojengwa bunge la ulaya mjini Brussels, Ubelgiji. Je ni ibada za Freemasons bungeni humo? Unalo jibu!
Je hayo ni maagizo ya mungu tunayemsadiki katika dini zetu? Na huyo mungu ndiye anayesema pale Brussels penye mwanamke aliyekataza ndipo mahali palipo na akili zaidi? Akili iliyofanya maangamizi ya Nagasaki na Hiroshima? Maangamizi ya Irag na Afghanistan?
Itazame Stempu ya 100 ya EU inavyofanana na sanamu hiyo. Sanamu ya mwanamke huyo imechorwa katika jengo hilo la bunge!. Hii ni imani za mwenyezi mungu? Na kwanini alimfunulia Yohana kama makatazo lakini ikachukuliwa alama poa kwa kizazi cha Freemasons Hall?
Vilevile ukiitazama Sarafu mpya ya jumuiya ya ulaya ina alama ya mwanamke aliyeketi juu ya mnyama kama awali. Je Yohana anatufunulia mwisho wa dunia kwa kutonyesha kizazi cha shetani? Je Papa Yohane Paulo I alitaka kupambana na hayo? Mbona Malkia Elizabeth alimtunuku Jayantilal Kashavji au Andy Chande? Hapo ndipo utaona tofauti yake.
Je Papa Yohane Paulo I angeliweza nguvu ya kizazi cha gizani cha Opus Dei ndani ya kanisa la Vatican?. Pamoja na kumwondoa Papa Yohane Paulo I katika freemasons, lakini wamezagaa ndani ya Vatican kwa kushirikiana na Mafia. Je kwani Papa hafahamu kazi halisi za Opus Dei?
Je ni kizazi cha shetani cha Freemasons? nimerudia baadhi ya hoja tulizojadili ili kuwaweka sawa wasomaji wapya na wengine kuhusu Freemasons ambao wamejikita katika misikiti, makanisani na katika shughuli za kitaifa zinazowakusanya watu. Nawashukuru wasomaji wanaohitaji tuandike kitabu, tutaelezana hilo. Freemasons ni nani?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment