KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Noti mpya zachanganya watu –Dar


KATIKA hali isiyo ya kawaida wafanyabiashara wengi wameonekana kuzigomea noti mpya wanazopewa na wateja wao kwa kuogopa huenda wanafanyiwa utapeli.
Hali hiyo imejitokeza ndani ya wiki hii tokea kuanza kuonekana mitaani kwa noti hizo Januari 8 mwaka huu.

NIFAHAMISHE ilishuhudia jana mfanyabiashara mmoja mlemavu wa miguu anayejishughulisha na uuzaji wa vocha akigomea noti ya shilingi elfu moja kwa kudhani huenda kijana anayehitaji vocha alikuwa akimfanyia uhuni kwa kumpa noti bandia.

Juhudi za kijana huyo kumfahamisha mfanyabiashara huyo ziligonga mwamba hadi mwandishi wa Nifahamishe alipoamua kumfahamisha mfanyabiashara huyo kuwa aipokee noti hiyo kwani haina tatizo lolote na kumuelewesha kuwa noti hiyo ndio miongoni mwa noti mpya zilizotangazwa zitatolewa mwanzoni mwa mwaka huu.

Hali hiyo pia ilijitokeza maeneo ya Tandika baada ya baba mmoja kufika na noti ya shilingi elfu tano ili kununua nguo ya mtoto katika moja ya duka na kuambiwa abadilishe awape noti nyingine mbali na hiyo.

Hata hivyo baba huyo kwa bahati alikuwa na noti nyingine ya zamani aliwapatia wafanyabiashara hao na kupatiwa nguo hiyo.

No comments:

Post a Comment