KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Wamachinga wa kichina wafukuzwa nchini


WIZARA ya Viwanda na Biashara imetoa tamko la kuwataka wafanyabiashara ndogondogo wa kichana wanaoendesha shughuli zao nchini kuondoka mara moja na kuwapisha wazawa kuendesha shughuli hizo.
Tamko hilo lilitolewa na wizara hiyo kuwataka wafanyabishara hao kuondoka mara moja nchini.

Naibu Waziri wa wizara hiyo. Bw. Lazaro Nyalandu, aliyasema hayo jijini Dar es Salam kwenye mahojiano maalum na kutoa msimamo huo wa wizara juu ya wafanyabiashara hao.

Nyalandu alisema kuwa, wizara yake imetoa muda kwa wafanyabiashara hao kuondoka nchini na watakaokiuka watachukuliwa hatua za kisheria zilizowekwa na serikali.

Amesema muda wa wiki tatu umetolewa kwa wafanyabishara hao wawe wameondoka nchini kwa kuwa wameonekana kusambaa kila kona ya nchi wakiuza bidhaa ambazo zimeonekana hazina ubora wa kutosha kwa watumiaji wa bishaa hizo.

Katika kuhakikisha hilo serikali kupitia wizara hiyo inaandaa mikakati maalum kuhakikisha wafanyabiashara hao wanaondokan nchini.

No comments:

Post a Comment