KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Nkya atembelea Mwanayamala


NAIBU WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Lucy Nkya jana alitembelea hospitali ya Mwananyamala kukagua utendaji wa hospitali hiyo pamoja na kukagua chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo.
Nkya alitembelea hospitali hiyo kwa kusikitishwa na tukio lililotokea la vichanga kuzikwa katika shimo moja waliokufa ndani ya hospitali hiyo.

Nkya amesema kutokana na kitendo hicho Wizara yake imeahidi kuwashughulikia waharifu wahusika wa kitendo hicho kilichofanywa kinyume na sheria.

“Nimesikitishwa kwa kudhalilishwa kwa watoto wale kwani ni kitendo cha kinyama, wahusika watashughulikiwa” alisema Nkya

No comments:

Post a Comment