KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, January 29, 2011

Maandamano yafanyika Yemen


Maelfu ya watu wameandamana mjini Sanaa nchini Yemen.


Wafuasi na wapinzani wa serikali ya Yemen waandamana
Wapinzani na wafuasi wa rais Ali Abdullah Saleh waliandamana katika maeneo tofauti ya mji huo.


Mkutano wa upinzani uliendelea kwa saa chache lakini watu wanaoongoza maandamano walisema huu ni mwanzo tu.

Wapinzani wa rais Ali Abdullah Saleh wanataka mabadiliko ingawaje baadhi walisema hawataki kiongozi huyo kuondoka madarakani.

Rais Saleh amekuwa madarakani kwa miaka 32. Wafuasi wake walijitokeza mitaani mjini Sanaa wakisema pia wanataka mabadiliko chini ya uongozi wa rais Saleh.

Baada ya waandamanaji kuondoka, baadhi ya wanafunzi waliamua kubaki wakisema hawataondoka hadi pale rais Saleh atakapoondoka mamlakani

No comments:

Post a Comment