KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Mwanafunzi kidato cha sita afa wakati akifanya mtihani


MWANAFUNZI Shamsa Jongo wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Jitegemee ya jijini Dar es Salaam, amefariki dunia ghafla wakati alipokuwa darasani akifanya mtihani wa kumaliza kidato hicho.
Tukio hilo lilitokea juzi shuleni hapo majira ya mchana, wakati akiwa katika chumba cha kufanyia mtihani wa kuhitimu.

Mwanafunzi huyo alidondoka ghafla akiwa katika chumba cha kufanyia mtihani na kufariki dunia papohapo.

Mwanafunzi huyo alikuwa akifanya mtihani wa somo la General Studies.

Hata hivyo walimu shuleni hapo walisema mwanafunzi huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo mara kwa mara.

Mitihani ya kidato cha sita ilianza Februari 7 mwaka huu, nchini kote

No comments:

Post a Comment