KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

1,200 wasimamishwa UDSM


WANAFUNZI wapatao 1,200 wa shahada ya kwanza ya Uhandisi na Teknolojia (COET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wamesimamishwa masomo yao baada ya kuingia katika mgomo wa siku tano na kusababisha vurugu chuoni hapo.
Taarifa hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo.

Mukandara amesema kuwa wanafunzi hao wamekuwa wakisababisha vurugu chuoni hapo kuanzia Februari 4 na kuvuruga ratiba ya masomo,waliwatishia wahadhiri ikiwemo na kuwazuia wenzao wasifanye mitihani chuoni hapo.

Alifafanua kuwa chanzo cha wanafunzi hao kufanya fujo walitaka mwanafunzi mwenzao aachiwe aliyekutwa na kartasi ya majibu na msimamizi na alipotakiwa kuionyesha aliimeza kwa kupoteza ushahidi, na mwanafunzi huyo kamati aliamuru imsimamshe masomo.

“Kitu walichokifanya hakikubaliki, kwa mujibu wa kanuni za masomo, watarudi majumbani kwao kwa muda usiojulikana, hatuwezi kuendesha chuo kwa kushinikizwa,” alisema Profesa Mukandala

No comments:

Post a Comment