KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Mwanafunzi Darasa la Tano Adaiwa kuwa Mchawi


MWANAFUNZI mmoja [jina linahifadhiwa] wa darasa la tano katika shule ya msingi Liwiti iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam amedaiwa kuwa ni mchawi baada ya mwanafunzi mwenzake kuumwa kutokana na kauli alizomtishia.
MWanafunzi huyo inadaiwa kuwa anachezea wanafunzi wenzake katika mazingira ya kimazingara akiwemo na mwalimu mmoja kuumwa kwa kutishiwa na mwanafunzi huyo.

Imedaiwa kuwa mwanwafunzi huyo amekosesha amani shuleni hapo kutokana na kauli zake za vitisho za imani za kishirikina anazozitoa kwa walimu na wanafunzi shuleni hapo.

Imedaiwa na walimu na wanafunzi kutoka shuleni hapo kuwa awali mwanafunzi huyo aliadhibiwa na mwalimu wake wa darasa kwa kutofanya kazi aliyopewa na mwalimu huyo na mwanafunzi huyo bila woga alimwambia mwalimu huyo kesho yake (alhamisi ya wiki iliyopita) kuwa “Utaona kama utaweza kuja kazini, nitakuonyesha”

Mwalimu huyo siku iliyofuatia hakuweza kuonekana shuleni hapo kutokana na ripoti kuwa alikuwa akimwa na kudaiwa hadi jana mwalimu huyo alikuwa bado hajaanza kazi kwa kudai kuwa anaumwa.

Mara ya pili imedaiwa kuwa alikwaruzana na mwanafunzi mwenzake aliyetambulika kwa jina la Warda Jamal,kumwambia kauli ile ile na kuongeza "Utaona kama utaamka nitakufanyia kitu kibaya kama mwalimu wako”.

Mara baada ya kutamkiwa kauli hiyo na mwanafunzi huyo, Warda alikwenda kuripoti tukio hilo kwa mwalimu mkuu.

Katika hali ya kushangaza imedaiwa kuwa mwanafunzi huyo alikubali kutoa kauli hizo na alikiri kuwa alikuwa akishiriki vitendo vya kishirkina kwa kushirikiana na bibi yake.

Mwanafunzi aliyetamkiwa maneno hayo siku iliyofuata afya yake haikuwa nzuri na mzazi wake alikuja shuleni kuthibitisha hali ya mtoto wake.

Hata hivyo uongozi wa shule hiyo umedai kuwa mwanafunzi huyo anayedaiwa kuwa mchawi alipewa barua ya wito amuite bibi yake aje shuleni lakini imedaiwa bibi huyo alikaidi kufika shuleni hapo jana na hatua zaidi zinachukuliwa.

Kufuuatia hali hiyo shuleni hapo wazazi wamekuwa katika hofu kubwa na wengi wakielezea kutaka kuwahamisha watoto wao kuwapeleka shule nyingine huku wengine wakiwazuia watoto wao wasifike shuleni hapo.

No comments:

Post a Comment