KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Ajilipua ndani ya Uwanja wa Ndege na Kuua Watu 35


Mtu mmoja amejitoa mhanga kwa kujilipua na bomu ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moscow nchini Urusi na kupelekea vifo vya jumla ya watu 35 na kujeruhiwa kwa watu zaidi ya 100.
Ilikuwa ni hali ya kutisha kwenye uwanja wa ndege mkubwa kuliko yote nchini Urusi wa Domodedovo Airport uliopo kusini mwa mji mkuu wa nchini hiyo Moscow.

Muda mfupi baada ya mtu mmoja kujilipua ndani ya uwanja wa ndege huo kwenye sehemu ya kupokea abiria wanaowasili ilikuwa haijulikani yupi yupo hai au yupi amefariki kutokana na mazingira ya kutisha iliyojitokeza.

Rais wa Urusi Dmitry Medvedev aliitisha kikao cha ghafla ambapo alisema kuwa tukio hilo lililotokea leo jumatatu kuwa ni la kigaidi na kuagiza ulinzi mkali kwenye viwanja vya ndege na stesheni za treni.

"Leo saa kumi na nusu (kwa saa za Urusi), mlipuko umetokea kwenye uwanja wa ndege wa Domodedovo Airport,", ilisema taarifa ya kikosi cha upelelezi cha Urusi.

Maafisa wa Urusi walisema kuwa mlipuko huo ulitokea kwenye eneo la kuchukulia mizigo kwenye sehemu ya kupokea abiria wanaowasili.

Watu 35 wamefariki na wengine 130 wamejeruhiwa katika mlipuko huo ambapo 20 kati yao hali zao ni mbaya sana.

Polisi wa Urusi wameanzisha uchunguzi wa mlipuko huo ambapo taarifa za awali zimeonyesha kuwa kuna mtu alijitoa mhanga kwa kujilipua mwenyewe ndani ya uwanja huo wa ndege

No comments:

Post a Comment