KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 12, 2011

Askari athibitisha Jerry alivyofika hotelin kwenda kuchukua rushwa


SHAHIDI wa nne katika kesi ya kupokea rushwa ya shilingi million 10, askari Issa Chabu (37), ametoa ushahidi wake jana mahakamani na kuthibitisha mshitakiwa Jerry Murro mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) alivyokwenda kupokea rushwa
Akitoa ushahidi huo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mbele ya Hakimu Mkazi Gabriel Mirumbe, alidai kuwa baada ya mlalamikaji kutoa taarifa hiyo polisi walipewa maelekezo kwa mkuu wake wa kituo na waliweza kufika mahali walipoahidiana na Wage kuja kuchukua fedha alizobakisha na Murro

akiwa na wenzake wawili waliojitambulisha kama wanatokea taasisi TAKUKURU na walifika mahali hapo majira ya saa 8 mchana bila kutambua kuwa kulikuwa na askari ambao ni wao.

Alidai siku hiyo Wage aliwasiliana na Muro na walikubaliana wakutane kwenye mgahawa wa City Garden karibu na klabu ya Bilcanas ili ampatie fedha hizo, na kudai Muro alikubali na alifika kwenye mgahawa huo ambao maaskari walikuwa wamejipanga kumkamata nje ya mgahawa na wengine ndani.


Aliendelea kutoa ushahidi wake kuwa, Muro akiwa kwenye gari bila kujua mtego huo alimpigia Wage simu kuwa atoke nje ya mgahawa huo na alipotoka alimuoneshea ishara aliko ili aende na Murro kabla hajaingia ndani alishtuka na kutaka kuondoka lakini askari walimpa ishara asiondoe gari.

Na alimuuliza kama anamfahamu wage lakini alikana na walimchukua hadi kituo cha polisi.

Leo ni muendelezo wa mfululizo wa ushahidi dhidi ya kesi hiyo

No comments:

Post a Comment