KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Muigizaji Clooney apata malaria Sudan

George Clooney


Muigizaji wa Hollywood George Clooney alipata malaria alipotembelea Sudan mapema mwezi huu, lakini kwa sasa amepona.

Clooney mwenye umri wa miaka 49 hutembelea mara kwa mara nchi hiyo iliyopo barani Afrika kwa ajili ya kueneza zaidi taarifa za eneo lenye mgogoro la Darfur.

Alisema kwa uzoefu wake binafsi imeonyesha kuwa dawa muafaka inaweza kubadili "hali mbaya inayoweza hata kuua" na kuwa "siku 10 ambazo si nzuri badala ya kifo."

Msemaji wake Stan Rosenfield alisema hii ni mara ya pili kwa Clooney kupata maradhi hayo.

Muigizaji huyo anatarajiwa kujadili hali yake hiyo na kazi yake barani Afrika katika kipindi cha Piers Morgan cha CNN siku ya Ijumaa.

No comments:

Post a Comment