KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Korea kusini yawaokoa mateka baharini



Choi Young
Makamanda wa jeshi la wanamaji la Korea kusini wamevamia meli ya mizigo iliyokuwa imetekwa na maharamia katika bahari ya Arabia.

Lt Jenerali Lee Sung-ho alisema mabaharia wote 21 wa meli ya Samho-Jewelry inayomilikiwa na Korea kusini wameokoloewa.

Jeshi hilo la majini limesema wanane miongoni mwa maharamia waliuawa na watano wamekamatwa.

Korea kusini hufanya doria ikiwa ni sehemu inayohusisha mataifa mengi ya kupinga uharamia eneo hilo- ambapo ilipeleka meli ya kivita baada ya meli hiyo kutekwa siku ya Jumamosi.

Shughuli hiyo ya uokoaji ilifanyika takriban kilomita 1,300 kutoka pwani ya Somalia na imeelezwa na Lt Jenerali Lee kama "shughuli ya kijeshi iliyo bora".

Samho Jewelry yenye tani 11,500 ilikuwa imebeba kemikali kutoka muungano wa Imarati kuelekea Sri Lanka ilipotekwa baina ya maji ya Oman na India.

Mapema wiki hii, Rais Lee Myung-Bak aliliambia jeshi hilo kuchukua "hatua zozote ziwezekanazo" ili kuwaokoa Wakorea kusini wanane, Waindonesia wawili na raia wa Burma 11 waliokuwa kwenye meli hiyo.

Manowari ya Choi Young ilikuwa ikiilinda hiyo meli kwa takriban wiki nzima, na jeshi hilo limesema maharamia hao walionekana kupunguzwa nguvu na muda wote wa kukimbizana.

No comments:

Post a Comment