KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Mtoto wa Nje ya Ndoa Kuivunja Ndoa Hii ya Miaka 15


NDOA iliyodumu kwa muda wa miaka kumi na tano iko mbioni kuparaganyika baada ya mume kubaini mtoto mmoja kati ya watatu si wake.
Mume huyo [jina linahifadhiwa] amelazimika kutinga ukweni kutoa siri hiyo na kuacha watu wakiwa hawana nguvu kutokana na gunduliko hilo.

Imedaiwa kuwa mume huyo alishtuka miezi mitatu nyuma baada ya kugundua kuwa mke wake siku za nyuma alikuwa na mahusiano na mwanaume mwingine ambaye ni rafiki yake na alishtushwa na baadhi ya marafiki zake wengine kutokana na ufisadi wa mke wake.

Hata hivyo mara kwa mara alikuwa akisikia mwanaume huyo akiwasiliana na mke wake na kumuuliza kuwa mtoto huyo alikuwa akiendeleaje bila kutambua kuwa alikuwa ni rafiki yake.

Akiongea na Nifahamishe mume huyo alidai alijipanga na kuanza zoezi la kwenda kufanya vipimo vya kubaini hilo kwa mtoto mmoja mmoja bila ya mkewe huyo kujua zoezi hilo.

Alidai katika vipimo hivyo alibaini kuwa mtoto wa pili kati ya watoto watatu mwenye umri miaka sita kipimo kilionyesha si wake kwa mujibu vipimo.

Alidai kwa kuwa hakuweza kuamini moja kwa moja alienda hospitali nyingine aliyoitaja jina, na huko pia kipimo kilionyesha kuwa si mtoto wake kwa mujibu wa kipimo hiko.

Alidai awali wakati wanaoana alikuwa akifanya kazi katika shirika moja binafsi hapa nchini, na baadae aliacha na kuanza biashara zinazomfanya asafiri mara kwa mara.

Alidai aliweza kutoa taarifa hiyo kwa kaka zake ili wampe ushauri bila ya mke wake kujua na baadae alimbainishia mke wake na kumtaka mtoto huyo ampeleke kwa baba yake kwani hakuwa wake na kumtaka mke wake nae ahamie huko kwani alikuwa hamfai tena.

Hata hivyo mwanamke huyo alikana na kudai haikuwa kweli ndipo alipomuonyehsa vipimo hivyo.

Mwanzoni mwa wiki hii suala hilo lilianza kujadiliwa kuangalia uwezekano wa kuwaweka sawa wanandoa hao.

Alidai mtoto wao wa kwanza ni wa kiume [11], wa pili wa kike [6] na wa tatu wa kike [2].

Muendelezo wa habari hii utaendelea kuchapishwa.

No comments:

Post a Comment