KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, January 29, 2011

Ajiua baada ya kufeli kidato cha nne


MWANAFUNZI Diana Roman (18) mkazi wa Kibamba jijini Dar es Salaam, aliyehitimu katika Shule ya Sekondari Yusuph Makamba amejiua kwa kughadhibika na majibu yaliyomuonyesha amefeli matokeo ya kidato cha nne.
Diana aliamua kunywa sumu ya dawa ya Kunguni baada ya kughadhibika na matokeo hayo.

Taarifa ilisema kuwa, siku ya tukio marehemu alikuwa ametoka kusali na aliingia chumbani kwake na kuamua kujifungia na kunywa sumu ya Kunguni.

Ilidaiwea kuwa baada ya muda mama yake aliyetambulika kwa jina la Anna aliingia chumbani kwake na kumkuta akiwa amelala chini ndipo aliposhtuka na kuangalia juu ya kabati hakuikuta sumu hiyo mahali alipokuwa ameihifadhi.

Mama wa marehemu huyo alidai kuwa Diana awali aliwahi kunywa sumu hiyo na walimuwahi kwa kumnyang’anya na siku hiyo ndipo alikunywa bila kuonekana na kupoteza uhai wake.

Imedaiwa juhudi za karibu hazikufanikiwa kuokoa maisha ya Diana kwa kuonyesha juhudi za kumpa maziwa lakini sumu hiyo iliweza kummaliza na alifariki wakati walipokuwa wakimkimbiza hospitali ya Tumbi.

No comments:

Post a Comment