KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, January 29, 2011

Mgomo wakwamisha usafiri wa treni za mjini , Ureno
Mgomo wa wafanyakazi wa treni za mjini umeanzisha wiki ya migomo ya wafanyakazi wa sekta ya umma nchini Ureno, ambao wamekasirishwa na upunguzaji wa mishahara uliotokana na serikali kutokuwa na fedha. Mfumo wa treni za mijini ulishindwa kabisa kufanyakazi leo Jumatatu wakati wa asubuhi, na utafuatiwa na mgomo wa aina hiyo baadaye wiki hii kwa wafanyakazi wa huduma za reli, feri na mabasi. Upunguzaji wa mishahara katika sekta ya umma ni sehemu ya hatua za kubana matumizi zilizoanzishwa na serikali ya waziri mkuu Jose Socrates kupambana na mzigo mkubwa wa deni nchini Ureno.

No comments:

Post a Comment