KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Atupa mtoto kwa kudai ugumu wa maisha


MTOTO Yusuphu Juma [1] amekutwa ametupwa katika Mto Chiovi uliopo Morogoro kwa kudaiwa mama dyake alichoshwa na ugumu wa maisha.
Kamanda wa polisi mkoani humo Adolphina Chialo, alisema kuwa mwanamke huyo alidai kuwa alichukua uamuzi huo baada ya kuchoshwa na ugumu wa maisha wa kuela mtoto huyo.

Chialo alisema kuwa mwanamke aliyetambulika kwa jina la Faida Mwapili [26] mkazi wa Mbeya alimtupa mtoto huyo mtoni na kusababisha kifo chake na wanamshikilia.

Kamanda huyo alsiema unyama huo aliufanya Februari 13 mwaka huu, majira ya mchana katika mto huo.

Kamanda alsiema mwanamke huyo alidaiwa kuwa sababu nyingine aliyoiorodhesha ni kutelekezwa na mzazi mwenzake na kudai yeye hakuwa na uwezo wa kutosha kulea mtoto huyo



Tanesco yaomba radhi wateja



SHIRIKA LA UMEME TANZANIA [Tanesco] limewaomba radhi wateja wake kutokana na kukosekana kwa umeme kwa masaa kadhaa na kusababisha usumbufu.
Umeme huo ulikosekana juzi, jana katika maeneo mengi kutokana na kuanguka kwa nguzo nyingi za umeme zinazosambaza umeme katika maeneo hayo kutokana na mvua iliyonyesha juzi.

Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliangusha nguzo hizo na kuleta kadhia hiyo ya kukosa umeme katika maeneo mengi nchini.

Katika taarifa iliyotolewa jana na Afisa Uhusiano wa shirika hilo, bi. Badra Masooud amesema kukosekana kwa umeme huo ulitokana na mvua kubwa iliyoambatanaa upepo mkubwa.

Masoud alisema, tayari shirika hilo limesharudisha umeme maeneo mengi








Mbowe atangaza baraza dogo la mawaziri


KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani bungeni, ambaye pia ni Mbunge wa Hai [Chadema], Freeman Mbowe, jana alitangaza Baraza la Mawaziri Kivuli kutoka kambi ya upinzani.


Mbowe alitangaza baraza hilo kwa kudai lishirikiane vyema na baraza lililoundwa na Serikali ili liweze kufanya kazi kiufanisi.

Mbowe alitangaza baraza hilo lenye mawaziri 29 baada ya kupewa fursa ya kufanya hivyo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anna Makinda.

Mbowe ameunda baraza hilo kwa kudai chama hicho kimetimiza sharti ya kufikia asilimia 12.5 na kusema kufata kanuni za bunge.

Katika uteuzi wake Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto amemteua kuwa Katika Wizara ya Fedha na Uchumi, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amemteua Wizara ya Ardhi, Mbunge wa Ubungo John Mnyika atashughulikia Wizara ya Nishati na Madini


Ofisi ya Waziri Mkuu, amemteua Bi. Raya Khamis, (Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu wa Bunge) na Bi. Esther Matiko, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji.

Ofisi ya Rais Utawala Bora ni Bw. Said Arfi , Mahusiano na Uratibu Mchungaji Israel Natse , Bi. Suzan Lyimo Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Ofisi ya MAkamu wa Rais, Bi. Pauline Gekul , Muungano Bi. Grace Kiwelu

Mambo ya Ndani aliteuliwa Bw. Godbles Lema, Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Tundu Lissu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Ezekia Wenje.

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Bw. Joseph Selasini na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Silvester Kasulumbayi.


Wizara ya Kazi na Ajira, Bi. Regia Mtema, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Naomi Kaihula, Wizara ya Habari, Vijana na Michezo, Bw. Joseph Mbilinyi, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Mustapha Akunaay, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Opulukwa Meshack na Wizara ya Maji, Bw. Highness Kiwia.

Katika uteuzi huo Mbowe alibagua vyama vya vingine pinzani vinavyoshirki bungeni humo na kuchagua wabunge wanaotoka katika chama cha Chadema pekee


Spika awapa onyo wabunge



SPIKA wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Anna Makinda amewapa onyo wabunge kuitana majina yasiyo rasmi na kuwataka waitane kwa vyeo bungeni humo.
Spika ametoa onyo hilo jana bungeni baada ya kuona hali ya kuitana majina yasiyo rasmi inazidi kuongezeka bungeni humo.

Makinda amewakataza wabunge kuitaka kaka, dada, rafiki na majina mengine ambayo si rasmi wanapokuwa wakijibu maswali ama kuuliza maswali wakiwa bungeni.

“Naomba muitane majina rasmi na si kumuita mbunge ama Waziri ,napenda kujibu swali la kaka yangu Fulani, ama napenda kuumuuliza swali dada yangu Fulani swali la nyongeza ama kuitana rafiki, naomba majina hayo yasitumike tene” lazima bunge liheshimike" aliwaonya wabunge

Hivyo amewataka wabunge kuitana kwa vyeo vyao husika na si kuitana kiurafiki na kusema kuitana hivyo wanakiuka kanuni za bunge


MAULID kusomwa Leo usiku Mnazi Mmoja



BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), limesema kuwa Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), yataadhimishwa na kusomwa kesho usiku.
Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Suleiman Lolila, alisema Kitaifa siku hiyo itaadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal.


Alisema siku ya Jumatano itakuwa ni siku ya mapumziko kwa wauminina kufafanua kuwa Baraza la Maulid litaanza kusomwa kuanzia majira saa 10.00 alasiri katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.

Alisema katika baraza hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

Hivyo aliwatakia Waislamu kote nchini kusherehekea sikukuu hizo salama na kuwataka washerehekea katika maandiko matakatifu na kuwataka wasome Quruani sanna kuachana na mambo yasiyo matakatifu






Mama Kikwete anusurika ajalini

MKE wa Rais, Mama Salma Kikwete jana alinusurika kifo baada ya msafara wake kupata ajali iliyosababishwa kugongana kwa magari matatu katika eneo la Ruvu Darajani mkoani Pwani.


Katika ajali hiyo dereva wa gari lililokuwa likiongoza msafara aliyetambulika kwa jina la Ramadhan Mkoma (58) alifariki dunia papohapo na majeruhi wengine 14 kukimbizwa katika Hospitali ya Tumbi na baadae watatu hali zao zikawa mbaya zaidi na walikimbizwa Hospitali ya TaifaMuhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Bw. Absalom Mwakyoma, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 6:00 mchana eneo hilo na kufafanua kuwa Mama Kikwete alikuwa akitokea Dar es Salaam kwenda nyumbani kwake Msoga kwa mapumziko.

Kamanda huyo alifafanua kuwa, ajali hiyo ilisababishwa na basi la abiria la Moro Best T 267 BHC lililokuwa linatoka Mpwapwa kwenda Dar es Salaam kugonga basi lingine dogo aina ya Toyota Hiace lililokuwa limeegeshwa pembeni kupisha msafara huo.



Hivyo mara baada ya basi hilo kugonga basi hilo lililoegesha pembeni kupisha msafara huo ilisbabisha basi hilo kuserereka na kugonganga uso kwa uso na gari lililokuwa likiongoza msafara huo





Wafanyakazi wa umma wagoma nchini Misri



Watumishi wa umma wanaogoma Misri

Maelfu ya wafanyakazi wa umma nchini Misri, wameitisha maandamano ya kitaifa kupinga mazingira mabaya ya kazi na pia mishahara duni.

Wafanyakazi hao wamepuuza wito wa viongozi wa kijeshi nchini humo wa kusitisha maandamano hayo ambayo yameathiri uchumi wa taifa hilo kwa kiasi kikubwa.

Waandamanaji wapya wamefurika bustani ya Tahrir, baada ya wanajeshi kufanikiwa kuwatimua waandamanaji wengine waliokuwa wamepiga kambi katika bustani hiyo katika maandamano yaliyopelekea rais Hosni Mubarak.

Huku hayo yakijiri, utawala wa nchi hiyo umesema kura ya maoni kuhusu katiba mpya, nchini humo itaandiliwa katika kipindi cha miezi miwili ijayo na kwamba viongozi wa upinzani watajumuishwa katika serikali ya mpito.

Mataifa kadhaa barani ulaya yamethibitisha kupokea ombi kutoka kwa utawala wa kijeshi nchini Misri wa kuzuia mali inayomilikiwa na maafisa wakuu wa serikali iliyoondolewa madarakani, iliyoongozwa na Hosni Mubarrak.



Marekani yaunga maandamano nchini Iran




Maandamano ya raia nchini Iran
Waziri wa Mashauri ya nchini za kigeni wa Marekani, Hillary Clinton, amewapongeza waandamanaji wanaopinga serikali nchini Iran.

Waandamanaji hao wamekabiliana vikali na maafisa wa usalama katika mji mkuu wa Tehran huku maandamano hayo yakiendelea kuongezeka.

Bi Clinton, amesema maandamano hayo ni ushahidi kamili, juu ya ujasiri wa watu wa Iran, ambao kwa sasa wanakabiliana na serikali ambayo imekuwa ikiunga mkono maandamano nchini Misri, kutokana na unafiki wake.

Raia wa nchi hiyo wameandamana katika sehemu mbali mbali za mji mkuu wa wa Tehran na sehemu zingine nchini humo.

Shirika moja la habari la nchini Iran, limesema mtu mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi katika machafuko hayo.








Kampuni ya Chevron yatozwa faini ya $8B




Uchafu unaodaiwa kusababishwa na kampuni ya Chevron


Mahakama moja nchini Ecuador, imetoza kampuni ya mafuta ya Chevron faini ya $8B kwa kuchafua mazingira katika eneo kubwa la Amazon nchini humo.

Wakili wa walalamishi, Pablo Farjado, alilaumu kampuni ya Texaco iliyoungana na Chevron mwaka 2001 kwa kuyachafua hali ya mazingira katika misitu Kaskazini mwa Ecuador kuanzia mwaka 1972.

Kampuni hiyo ya Chevron imesema inajadili uwezekano wa kukata rufaa.

Farjardo amesema kuwa mimea iliharibiwa na maji ya kunywa kuchafuliwa kitendo ambacho kilisababisha raia katika eneo hilo kukumba na mateso mengi.

Chevron, kwa upande wake, imesema kuwa uamuzi huo wa mahakama ni mgumu kutekeleza na kwamba watakata rufaa.

Msemaji wa chevron, Kent Robertson, aliambia BBC kuwa Texaco ilisafisha maeneo yote yaliyochafuliwa baada ya kumaliza shughuli zake nchini Ecuador na inalaumu kampuni ya serikali ya Petro-Ecuador kwa kuendelea kuchafua maeneo hayo baada ya Texaco kuondoka








Maandamano Misri yawa madai ya mishahara


Maandamano mapya na migomo imeikumba Misri, kufuatia wafanyakazi kudai mishahara mizuri zaidi na mazingira bora ya kazi kutoka kwa watawala wapya wa kijeshi.





Wafanyakazi wakifanya mgomo Cairo


Wafanyakazi wa benki, usafiri wa umma na utalii waliandamana mjini Cairo, siku 18 baada ya maandamano yaliyofanikiwa kumuondoa Rais Hosni Mubarak.

Katika taarifa kupitia televisheni, jeshi limewataka wafanyakazi wote kurejea kazini.

Mapema, eneo la wazi la Tahrir, waandamanaji waliondolewa, lakini muda mfupi baadaye mamia walirejea, akiungwa mkono na polisi waliokuwa wakinung'unika.

Mamia ya polisi wenye sare na wengine wasio kuwa nazo, waliandamana kuelekea Tahrir, huku wakipiga kele: "Sisi na raia ni sawa" na kuahidi "kuenzi mashujaa wa mapinduzi".

Wamesema wamelazimishwa kufanya matendo kinyume na matakwa yao, katika kutumia mguvu dhidi ya waandamanaji, mapema wakati maandamano yakianza.









Italia yajitahadharisha na wahamiaji


Wahamiaji wa Tunisia


Serikali ya Italia inajitahidi kukabiliana na mgogoro uliopo katika kisiwa kidogo cha Lampedusa baada ya wahamiaji 1,000 kuwasili kutoka Tunisia.

Kituo kimoja kilichoandaliwa mahsusi kwa ajili ya watu 850 kimeripotiwa kufurika.

Tunisia imeikatalia Italia kusambaza polisi wake kwenye eneo lao.

Zaidi ya wahamiaji 4,000 wanaripotiwa kuwasili Lampedusa katika siku chache zilizopita.

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Baroness Ashton kwa sasa yupo Tunis kujadili suala hilo.

Waziri wa mambo ya nje wa Italia Franco Frattini naye anatarajiwa kufika Tunis siku ya Jumatatu.

Gazeti la Italy La Repubblica limeripoti kuwa alijadili kuhusu mmiminiko huo wa wahamiaji na Lady Ashton na kutoa wito wa shirika la mipaka la Umoja wa Ulaya Frontex kujihusisha, kusaidia kupiga doria kwenye maji ya Lampedusa.

Siku ya Jumamosi Italia ilitangaza dharura ya masuala ya kibinadamu na kutoa wito wa kupata msaada kutoka Umoja wa Ulaya.

Msemaji wa shirika la kimataifa la uhamiaji, Simona Moscarelli, alisema Italia lazima iwahamishe wahamiaji kutoka Lampedusa kwenda upande wa bara wa Italia haraka iwezekanavyo




Jeshi lafuta bunge Misri

Utawala mpya wa kijeshi nchini Misri umesema unalifunga bunge la kuisimamisha katika ya nchi kwa muda.



Waandamanaji mjini Cairo


Katika taarifa kupitia televsheni ya taifa, baraza la juu la kijeshi limesema litakaa madarakani kwa miezi sita, au mpaka wakati utakapofanyika uchaguzi.

Bunge la sasa la Misri, limetawaliwa na wafuasi wa Rais Hosni Mubarak, ambaye aliondoka madarakani siku ya Ijumaa, kufuatia siku 18 za maandamano.


Waandamanaji katika eneo la wazi la Tahrir


Mapema kulikuwa na mzozano katika eneo la wazi la Tahrir, baada ya waandamanaji kugomea hatua za jeshi za kuwaondoa katika eneo hilo.

Polisi wa kijeshi wametaka mahema kuondolewa katika eneo hilo ambalo ni kitovu cha maandamano yaliyosababisha kuondoka kwa Bw Mubarak.

Mwandishi wa BBC Wyre Davis aliyeko mjini Cairo anasema hali katika eneo hilo la wazi imekuwa kama mvutano wa kirafiki, lakini wandamanaji wamesema wataendelea kusalia hapo hapo


Polisi wa kijeshi wakiwa na waandamanaji


Taarifa ya jeshi ilioyosomwa kupitia televisheni ya taifa siku ya Jumapili imesema itasitisha katiba iliyopo na kuunda kamati itakayoandika muswada mpya wa katiba, kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni.

Katiba ya sasa inazuia vyama ving vya kisiasa na makundi kushiriki katika uchaguzi, na hivyo kufanya bunge la nchi hiyo kujaa wafuasi wa chama cha National Democratic, ambacho kinamtii Bw Mubarak.

Mwandishi wetu anasema, tangazo hili jipya linamaanisha uchaguziutafanyika mwezi Julai au Agosti, badala ya Septemba kama ilivyokuwa imepangwa.











Mwanamke Mwenye Wivu Anyofoa Sikio la Mumewe




Mwanamke mmoja wa nchini ametupwa jela miezi 18 baada ya kuling'ata na kulinyofoa sikio la mpenzi wake baada ya kukasirishwa na kitendo cha mhudumu wa kike wa baa kumnunulia mumewe bia kama zawadi ya bethidei.
June Thomson mama wa watoto watano wa nchini Uingereza amehukumiwa kwenda jela miezi 18 kwa kitendo chake cha kukinyofoa kipande cha sikio la mumewe na kukitema chini na mbwa wao kukimeza.

June mwenye umri wa miaka 44 alikuwa baa na mumewe, Trevor Wainman, 45, wakati mhudumu wa baa alipomnunulia bia Trevor kama zawadi ya bethidei.

Waliporudi nyumbani, kutokana na wivu June alianza kumshambulia mumewe akihoji imekuwaje anunuliwe bia na baa medi.

Alimpiga ngumi za uso mumewe huku akimtupia maneno kabla ya kuling'ata sikio lake na kukinyofoa kipande cha sikio hilo.

Alikitema chini kipande hicho cha sikio na mbwa wao aliyepewa jina la Alfie alikipitia na kukimeza.

"Alinikandamiza na kuzamisha meno yake kwenye masikio yangu na kunyofoa kipande cha sikio langu, sijawahi kusikia maumivu kama yale katika maisha yangu, damu zilisambaa kila kona, ukutani na kwenye sakafu ilikuwa ni kama bomu limelipuka", alisema Wainman.

"Alinifanya nionekane kama vile nimegongwa na gari, ana wivu sana natamani nisingejuana naye maishani mwangu", aliongeza.

Uchunguzi wa polisi ulibaini kuwa mbwa wao ndiye aliyekimeza kipande cha sikio kilichonyofolewa.

Mahakama ilimuona June ana hatia na ilimhukumu kwenda jela miezi 18




Michelle Obama Awapiga Marufuku Binti Zake Kutumia Facebook


Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama amewapiga marufuku binti zake kujiunga na mtandao wa Facebook.
Pamoja na kwamba mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama amekuwa akisema kuwa anataka watoto wake waishi maisha ya kawaida kama watoto wengine, amewapiga marufuku watoto wake kujiunga na mtandao wa Facebook.

Akiongea kwenye kipindi cha televisheni cha Today show, ambacho alialikwa ili kuzungumzia kampeni yake ya kuwashawishi vijana kula vyema na kufanya mazoezi, Michelle Obama alijikuta akiulizwa maswali mengi kuhusiana na familia yake.

"Mimi sipendelei watoto kujiunga na mtandao wa Facebook, sio kitu wanachokitaji kwa wakati huu", alisema bi Obama.

Michelle Obama alisema kuwa hatawaruhusu watoto wake Sasha mwenye miaka 9 na Malia mwenye miaka 12, wajiunge na mtandao huo unaoziunganisha jamii mbalimbali duniani.

Aliongeza kuwa kwa kutegemea na umri wao na muda ambao Obama atakuwa madarakani kama ni miaka miwili ijayo au sita ijayo, asingependelea kuwaona binti zake wakijiunga na mtandao huo.

Hata hivyo bi Obama hakuelezea kama uamuzi wake huo unatokana na wasiwasi wa baadhi ya watu kuhusiana na watoto kujiunga na mtandao wa Facebook ambao una jumla ya wanachama milioni 600 duniani.





NATO yakamata mashua ya maharamia


Kikosi cha NATO kinachoshughulikia tatizo la uharamia kimesema, meli yao ya kivita imeinasa mashua kuu ya maharamia karibu na mwambao wa Somalia

Meli ya kivita ya Denmark


Meli hiyo ya kivita kutoka Denmark ilifyatua risasi siku ya Jumamosi kama onyo na kuilazimisha mashua hiyo kusimama na mabaharia wake kujisalimisha.

Watuhumiwa kumi na sita waliokuwa kwenye mashua hiyo walikamatwa na silaha zilizokuwa zimefichwa humo kunaswa pia.

Mateka wawili raia wa Yemen waliokuwa ndani ya mashua hiyo pia waliachiwa.

'Mashua hizo zinawapa maharamia mahali pa kuegesha majini. Zinaleta tishio kubwa kwa meli za bidhaa,' Kamanda Haumann wa meli hiyo ya kivita ya HDMS Esbern Snare alisema.

Kikosi hicho cha NATO kilisema tukio hilo lililfanyika siku ya Jumamosi asubuhi wakati meli ya Denamark ilipokutana na chombo kilichokuwa kimebeba mashua ndogo nyepesi na kuwatilia mashaka.

Walishuku kuwa chombo hicho kilikuwa kimetekwa nyara.

Mamilioni ya dola

Jeshi la majini la Jumuiya ya Ulaya pamoja na kikosi cha NATO, wamekuwa wakisindikiza meli za bidhaa katika Ghuba ya Eden tangu mwaka wa 2008.

Mapema wiki hii, Umoja wa wamiliki wa meli za mafuta walisema maharamia kutoka Somalia wameziteka meli takriban ishirini na kuzitumia kuwashambulia mabaharia.

Maharamia wa Somalia wamepata mamilioni ya dola katika miaka ya hivi karibuni kwa kuziteka nyara meli za bidhaa karibu na Pembe ya Afrika, na kudai kulipwa fedha za kikombozi.

Somalia haijakuwa na serikali dhabiti tangu mwaka wa 1991 na haina uwezo wa kudhibiti tatizo hili la maharamia.







Watu 11 wamekufa katika mkanyagano kwenye mkutano wa kisiasa nchini Nigeria


Rais Goodluck Jonathan

Mkutano huo uliofanyika katika mji wa kusini wa Harcourt, ulikuwa sehemu ya mkutano wa kampeni wa rais Goodluck Jonathan, kabla ya uchaguzi wa mwezi April.

Uchunguzi

Watu wengine 29 wanasemekana kujeruhiwa katika mkutano huo, ambao ulifanyika kwenye uwanja wa michezo.

Rais Jonathan ameagiza kufanyika kwa uchunguzi na kusema tukio hilo lilikuwa "la kusikitisha, bahati mbaya na la kujutia," na kuongeza: "Naomboleza na wale wanaoomboleza."

Umati huo ulishituka, baada ya polisi kufyatua risasi hewani, kujaribu kutawanya watu katika milango ya kuingiliwa uwanjani, wakati watu wakitoka, kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo na kukaririwa na shirika la habari la Reuters.

"Kulikuwa na kundi kubwa la watu, na sehemu ilikuwa imejaa," amesema Ken Saro-Wiwa, msaidizi wa Rais Jonathan wa masuala ya kimataifa, ameiambia Reuters.

"Ni mwisho wa kusikitisha katika siku iliyoanza vizuri," amesema Bw Saro-Wiwa





Manispaa yaingilia sakata la kifo cha mzazi Ukonga




HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imeunda timu maalum kuchunguza chanzo cha kifo cha Sabela Mganga(31) aliyefariki katika zahanati ya CHO ya Ukonga Mazizini baada ya kujifungua watoto mapacha na kuzuiliwakwenda hospitali ya wilaya kutokana na deni li
Marehemu Sabela alizuiliwa kutoka katika zahanati hiyo kwenda kupata matibabu katika hospitali ya Amana kutokana na kudaiwa kiasi cha shilingi 155,800 kama gharama za kujifungua.

Marehemu alipelekwa katika zahanati hiyo tangu Februari 5 hadi 7 na kujifungua watoto mapacha na mara baada ya kujifungua watoto hapo aligundulika kuwa aliishiwa damu na daktari kutaka mama huyo apelekwe amana kwa matibabu zaidi.

Hivyo timu hiyo maalum imeundwa chini ya Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala na baadae ripoti hiyo kupelekwa kwa mkurugenzi na kutolewa rasmi.

Taarifa kutoka dnani ya familia hiyo inasema watoto hao mapacha wanaendela vizuri na mazishi ya mwanamke huyo yanatarajiwa kuwa kesho mkoani Dodoma

No comments:

Post a Comment