KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, February 16, 2011

Jeshi la Misri lataka mabadiliko



Misri

Baraza la jeshi linalotawala Misri limetangaza kuwa kazi ya kurekebisha katiba ya nchi hiyo inatakiwa kukamilika katika kipindi cha siku 10.

Kamati inayoongozwa na jaji aliyejiuzulu imepewa jukumu la kupendekeza mabadiliko ya kisheria.

Baraza hilo lilisitisha katiba iliyokuwepo mwanzo, ambayo ilifanyiwa marekebisho wakati Rais aliyondolewa Hosni Mubarak alipokuwa madarakani, iliyokuwa ikimpa uwezo mkubwa sana wa uongozi.

Bw Mubarak amejiuzulu wiki iliyopita baada ya kuwepo maandamano ya zaidi ya wiki mbili.

Baraza la jeshi la ngazi ya juu, ambalo limeshika hatamu baada ya Bw Mubarak kujiuzulu alisema, katiba hiyo itakayorekebishwa itapigiwa kura ya maoni baada ya kamati hiyo kutoa mapendekezo.

Wanachama wengine wa kamati hiyo ni wataalamu wa sheria ya katiba lakini pia imemhusisha kiongozi mwandamizi kutoka upinzani, the Muslim Brotherhood.

Mwandishi wa BBC Jon Leyne mjini Cairo alisema inaonekana baraza la jeshi linatimiza ahadi yake ya kukabidhi nchi kwa raia haraka iwezekanavyo.

Kasi hiyo itawapa uhakika upinzani, alisema, japo kutakuwa na wasiwasi iwapo ni jaribio la kuleta mabadiliko kwa haraka mno

No comments:

Post a Comment