KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 12, 2011

Mama aliyepoteza watoto wanne aanika siri ya hasira za mumewe


BI.PASKAZIA SIXBERT, mama aliyepoteza watoto wanne katika tukio la mauaji atoa siri iliyomfanya mume wake ashikwe na hasira na kuamua kuuwa watoto kisha mwenyewe kujinyonga.
Paskazia ambaye anayeishi kwa masikitiko makubwa baada ya kupoteza watoto wake aliweza kuimegea siri nifahamishe na kuweka uwazi huo.

Alidai kuwa mume wake alikuwa ni mtu mwenye hasira na wivu kupitwa kiasi na chanzo kikubwa na maujai hayo ni baada ya mume huyo kumkuta amesuka nywele kitendo ambacho alikwua hajakifurahia.

Alieleza kuwa, mara bada ya kumkuta amesuka nywele hizo alimuuliza ni nani alimruhusu asuke nywele bila idhini yake na ndipo ugomvi ulianza na kudhani pesa ya kusuka nywele hizo alipewa na mwanaume mwingine.

Nae aliweza kumjibu mumewe huyo na kumwambia kuwa alisuka nywele hizo kwa matakwa yake na alifanya hivyo ili aonekanane nadhifu kama wengine .

Alisema mara baada ya kumpa majibu hayo mume huyo alimvamia na kumng’ata katika kidole chake cha kushoto na aliweza kuking’ata na kufanikiwa kubaki nacho mdomoni kisha alikitema chini.

Alisema alimng’ata kidole hicho kwa kuwa alikuwa amevaa pete ambayo pia alimuuliza alikuwa ameitoa wapi, na kueleza kuwa damu nyingi zilianza kumtoka na kuamua kutoa taarifa hiyo kituo cha polisi na kuamua kurudi kwao na kesho yake ndipo aliposikia kuwa mumewe aliua watoto hao.

Alisema alianza kutokwa na damu nyingi na kuamua kwenda polisi kutoa taarifa na kupewa fomu ya matibabu PF3 na kwamba aliporejea nyumbani kwa wazazi wake, kesho yake alipata taarifa za mumewe kuwaua watoto wake na yeye kujinyonga.

Hata hivyo alibainisha kuwa Agosti mwaka jana ugomvi wa mara kwa mara ulikuwa ukitokea kati yao mumewe huyo akimtuhumu kumuibia fedha dukani kwake na kuamua kurudi nyumbani kwao kwa mapumnziko na alikutana nae siku ya tukio Karatu akiwa amesuka nywele hizo na kuchukia na kudhani pete hiyo alivalishwa na mwanaume mwingine

No comments:

Post a Comment