KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Baba akanyaga mwanae na gari, wanafunzi wapoteza maisha ufukweni


BWANA Joseph Maso [34] mkazi wa Kinyerezi Izimbili, Dar es Salaam, amemuua mwanawe mwenye umri wa mwaka mmoja kwa kumkanyaga na gari wakati akirudisha gari hilo nyuma nyumbani kwake.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 5 asubuhi nyumbani kwa Joseph.

Alisema wakati akirudisha nyuma gari hilo nje ya nyumba yake ndipo alimkanyaga mtoto wake ambaye alikuwa akicheza upande wa nyuma ya tairi upande wa kushoto wa gari hilo.

Alisema mtoto huyo aliyetambulika wka jina la Godfrey alifariki wakati akikimbizwa hospitali ya Amana kwa matibabu

Katika tukio jingine wanafunzi watatu wa kidato cha nne katika shule ya wasichana ya John Baptist iliyoko Boko jijini Dar es Salaam wamefariki dunia papo hapo baada ya kuzama katika maji wakati walipokuwa wakiogelea ufukweni.

Katika tukio hilo lililotokea jana majira ya jioni wanafunzi wengine watatu walizimia wakati wakiwa katika mazoezi ya viungo katika ufukwe wa Ununio.

Wanafunzi hao walikuwa wakiogelea ufukweni hapo na walizidiwa na kina kirefu cha maji na hatimaye kuzama na kupelekea kupoteza maisha.

Wanafunzi hao waliongozana na mwalimu wao alifahamika kwa jina la Philotheus Mayemba (32) wka ajili ya kwenda kufanya mazoezi ukukweni hapo ambapo imedaiwa ni utaratibu wa shule hiyo kila Ijumaa kwenda eneo hilo kwa ajili ya kwenda kufanya mazoezi ya viungo.

Hata hivyo imedaiwa kuwa wanafunzi hao waliamua kumtoroka mwalimu wao kukimbia mazoezi hayo ya viungo yaliyokuwa yanafanyika mchangani na kuamua kufanya ujanja kwenda kuogolea baharini .

Wanafunzi waliopoteza maisha katika tukio hilo ni Janeth Simkanga (17), Winifrida Kisaka (17) na Hosiana Ntui [18].

Waliokolea ni Joan Kayanda [17], Linda Emanueli (14) Eforti Fulijensi (14)

No comments:

Post a Comment