KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 12, 2011

Makinda akataa kambi mbili za upinzani


SPIKA wa Bunge, Anna Makinda amesema hakuna uwezekano wa kuwepo kwa kambi mbili za upinzani bungeni.
Alitoa ufafanuzi huo jana jijini Dar es Salaam, katika semina ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Alisema kwa mujibu wa sheria bungeni kunakuwa na kambi ya upinzani moja na alisema ni jambo lisilowezekana kuwa na kambi zaidi ya moja.

Aliwataka wabunge wa upinzani wakakaa pamoja na kunda kambi moja yenye nguvu ili upinzani uwe imara na uweze kuibana vilivyo serikali na wajenge mshikamano na kupanga mikakati yao kuliko wanavyolumbna sasa.

Alisema kambi ya upinzani bungeni inaundwa kwa asilimia 12.5 na hivyo chama cha chadema kimeonekena kufanikiwa kwa kuwa wametimiza sharti hilo

No comments:

Post a Comment