KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 12, 2011

Abiria watekwa waibiwa mali


KUNDI la watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameteka basi lililokuwa likisafirisha abiria la Kampuni ya Falcon na kupora mali na vitu vya thamani vya abiria hao.
Majambazi hao waliweza kwuajeruhi abiria na kuwaamuru watoke nje ya basi hilo huku wakiwapiga mapanga na kuwapiga mawe huku wakiwaamrisha wainue mikono juu huku wakitoka ndani ya basi hilo.

Mbali na kuwajeruhi abiria waliweza kumkata kata mapanga dereva wa basi hilo na hali yake ilidaiwa kwua mbaya na kupoteza fahamu kwa muda ule.

Tukio hilo lilitokea juzi, majira ya saa 5 usiku, katika eneo la kati ya Sekenke wilayani iramba mkoani Singida basi lililokuwa likifanya safari zake kati ya Kampala na Dar es Salaam.

Ilidaiwa kuwa basi hilo lilipomaliza kupanda mlima wa sekenke walikuta lori likiwa limeegeshwa katikati ya barabara hivyo dereva wa basi hilo alishindwa kupita kutokana na lori hilo lilivyoegeshwa.

Wakati dereva wa basi hilo akiwa amesimama kutafakari ni jinsi gani atapita mahali hapo ghafla kundi la watu wanaozidi saba wakiwa na mapanga, mawe na silaha nyingine walivamia basi hilo.

Waliwaamuru abiria kushuka na kila anayeshuka akabidhi fedha alizokuwa nazo na simu

No comments:

Post a Comment