KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, January 12, 2011
Majadiliano ya uteuzi wa Waziri Mkuu mpya kuanza Lebanon
Majadiliano yaliyo na azma ya kufanikisha uteuzi wa Waziri Mkuu mpya nchini Lebanon yataanza Jumatatu.Kwa mujibu wa Spika wa Bunge la Lebanon Nabih Berri,hatua hiyo inachukuliwa baada ya serikali ya Umoja wa kitaifa kuvunjika.
Wakati huohuo Umoja wa Ulaya umetoa wito wa suluhu ya mzozo huo wa kisiasa kupatikana na mkuu wake wa sera za nje Catherine Ashton ameusisitizia umuhimu wa majadiliano.Kwa upande wake Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amekilaani kitendo hicho.
Wanachama wa Hezbollah wa Kishia walijiondoa kwenye baraza la mawaziri hapo jana jambo lililomfanya Waziri Mkuu Saad Hariri kujiuzulu.Hata hivyo Rais wa Lebanon,Michel Sleiman amemuomba Saad Hariri kuendelea kukaimu majukumu ya Waziri Mkuu mpaka mwengine atakapoteuliwa.
Mgogoro huo wa kisiasa umechochewa na mitazamo tofauti kuhusu tume maalum inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa inayoyachunguza mauaji ya Rafiq Hariri yaliyotokea mwaka 2005.Hezbollah inayoungwa mkono na Syria na Iran imekuwa ikimshinikiza Saad Hariri kutoitambua tume hiyo ya uchunguzi.Kwa upande wake Israel iko chonjo na vikosi vyake viko tayari ili kuzuwia ghasia zozote endapo zitatokea na kusambaa hadi mipakani mwao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment