KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Iraq iliyo na demokrasia ndio la msingi,asema Biden



Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden amefanya mazungumzo na Rais wa Iraq Jalal Talabani akiwa katika ziara ya kushtukiza ambayo ni ya kwanza tangu uongozi kushika hatamu mpya nchini humo.Katika ziara yake hiyo,Joe Biden alisema kuwa Iraq iliyo na demokrasia na mafanikio ndilo jambo la msingi na muhimu kwa Marekani katika eneo hilo.

Kwa upande wake,Rais wa Iraq Jalal Talabani alimsisitizia kuwa Marekani ni mshirika wake wa karibu na anaamini kuwa usuhuba huo utaendelea hata baada ya wanajeshi wake kuondoka Iraq.Marekani imeshasema kuwa itawaondoa wanajeshi wake alfu 50 waliosalia Iraq ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.Pindi baada ya kikao chake na Joe Biden,Waziri Mkuu wa Iraq Nuri-al Maliki aliahidi kuwa nchi yake itapambana na changamoto ilizonazo ziwe za kiusalama,kisiasa au nyenginezo.

Makamu huyo wa rais wa Marekani alikutana pia na viongozi wengine wa Iraq akiwemo Iyad Allawi wa muungano wa Iraqiya unaoungwa mkono na Wasunni.

No comments:

Post a Comment